Raia wa Uingereza wametakiwa kuondoka mji wa Benghazi nchini Libya mara moja, baada ya kutokea vitisho dhidi yao.
Kwa mujibu wa maafisa wa wizara ya mambo ya nje
ya Uingereza, ubalozi wa Uingereza mjini Tripoli umeweza kuwasiliana na
raia wa uingereza na kwamba imepokea taarifa zao.Wizara ya mambo ya nje imekuwa ikiwashauri watu dhidi ya kusafiri kwenda Benghazi na maeneo mengine mengi ye Libya tangu mwezi Septemba.
Katika onyo lake la hivi karibuni kuhusu safari za nchini humo, wizara ya mambo ya nje imesema kuwa baada ya hatua ya jeshi la Ufaransa, kuingilia mzozo wa Mali kumekuwa na uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi, dhidi ya maslahi ya nchi za kimagharibi katika eneo hilo.
Pia kuna uwezekano wa kufanyika visa vya utekaji nyara nchini Libya.
Tarehe 11 mwezi Septemba mwaka jana, balozi wa Marekani Chris Stevens na maafisa wengine watatu , waliuawa kwenye mashambulizi hayo dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.
Balozi huyo alifariki kutokana na moshi mkubwa aliponaswa ndani, ya jengo lililokuwa linateketea baada ya watu waliokuwa wamejihami kuvamia ubalozi huo.
No comments:
Post a Comment