Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa leo ametembelea maonyesho ya Wiki ya Elimu yanayofanyikia katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Wiki ya Elimu kitaifa inaadhimishwa mkoani Dodoma kuanzia tarehe 03 Mei, 2014 na itafungwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, siku ya Jumamosi tarehe 10 Mei, 2014.
Waziri Kawambwa katika maonyesho hayo alitoa zawadi kwa wanafunzi wshindi wa uandishi wa insha kutoka katika shule za msingi na sekondari za manispaa ya Dodoma.
Washindi kwa upande wa sekondari ni: Mawazo Matukuta (Msalato), Frank Stanley (Dodoma) na Heavenlight Minja (Dodoma)
Washindi kwa upande wa msingi ni: Jakunda Mahoo (Santhome), Emmanuel Mgana (Mazengo) na Radhia Mswanyama (Martin Luther)
|
No comments:
Post a Comment