MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji
la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC
yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika
kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo
ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari,
zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo
walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo
ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya
kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro
pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini
Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Hata hivyo moto huo uliodumu kwa saa kadhaa ulifanikiwa kuzimwa ndipo juhudi za kuyatoa magodoro na mito yote ya makochi yaliyokuwemo ndani ya hifadhi ya mizigo ili kuhakiki uharibifu pamoja na kufanya tathimini kwa mali zilizo haribika. |
Kwa umakini zaidi kuhakiki moto huo. |
Wafanyakazi wa MSC wakitumia mashine maalumu ya kushushia mizigo ya kampuni hiyo wakitoa mabaki ya vitu vilivyounguzwa na moto. |
Ikumnbukwe kuwa Mv. Serengeti kwa sasa haiko shughulini na Mv. Bukoba ndiyo hivyo tena ilizama mwaka 1996 na mamia ya ndugu zetu.
Juhudi za ushushaji mizigo iliyoungua zikiendelea. |
Mmliki wa magodoro pamoja na mito ya makocho iliyoteketea kwa moto aliyejitambulisha kwa jina moja la Ogunya amesema kuwa amepoteza magodoro 180 pamoja na mito 80 katika tukio hilo. |
Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa
majini na nchi kavu(SUMATRA) kanda ya ziwa Josephat Loisimaye amesema
kuwa uzembe wa viongozi wa MSC ndio ambao ulisababisha kutokea kwa moto
huo.
Amesema kuwa viongozi wa MSC walipashwa kuchukua tahadhari mapema
kabla ya kuanza uchomeleaji katika sehemu ya Meli hiyo na kueleza kuwa
wanasubiri ripori ili waweze kuchukua hatua zaidi.
Hata hivyo Loismaye amesema kuwa Meli ya Mv Victoia iko salama na
itaendelea na safari zake kwenda Bukoba leo usiku kwa kuwa moto huo
haukuweza kuathiri mfumo wa injini ya Meli na kukipongeza kikosi cha
zimamoto kutokana na kufika mapema na kuzima moto huo vinginevyo Meli
hiyo ingeliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.
Habari Na Gsengo Blog Kwa Picha Zaidi Mtembelee Kwa Kubofya Hapa
No comments:
Post a Comment