Thursday, February 7, 2013

JK azindua utoaji wa Vitambulisho vya taifa katika viwanja vya Karimjee leo

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho cha Taifa katika hafla ilkiyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mke wa Rais Mama Salma Kikwete kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo huku Rais Kikwete akishuhudia.Kushot o Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa kitambulisho cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kitambulisho cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.Picha  na Freddy Maro  wa Ikulu

No comments:

Post a Comment