Thursday, February 7, 2013

MSANII WA FILAMU SHIJA AKIRI KUWA NI KWELI ANAOA ARUSHA SIKU SI NYINGI

SHIJA
Kupitia MTAA WA PILI ROUND II DJ HAAZU amepata kupiga Story mbili tatu na Msanii mkubwa wa Filamu TZ Deogratius Shija Maarufu kama Shija ambapo tulizungumzia kazi yake Mpya ambayo inawahusu sana Jamii haswa wale wanafunzi wa kike ambao wanasoma vyuo na kuwa na tabia za kuwa na wapenzi wengi na wana ndoa au wapenzi ambao wanaamini kuwa kumkomoa Mpenzi wako anayekusaliti dawa yake ni Kumsaliti nawe kwani mwisho wa Movie hiyo inayokwenda kwa Jina la BEAUTIFULL ambayo humo ndani pia kacheza marehemu John Maganga.

katika maelezo yake shija amesema movie hiyo wanategemea kuiachia Tarehe 14 Feb 2013 siku ya Valentine day na ni movie kali kwani tofauti na marehemu Maganga ambaye kamtaja kama msanii ambaye ameonyesha uwezo mkubwa sana kwenye filamu hiyo pia wapo wasanii wengine wakubwa Nchini kama Aunt Ezekiel, Mboto, Eisha Guet pamoja na yeye pia amecheza sin flani kama DJ.

Wakati tunapiga story mbili tatu jamaa nilimuuliza pia kuhusu tetesi za yeye kuja kuoa Arusha kwamba ameshapata mchumba na wanataka kufunga ndoa ambapo jamaa alifunguka bila wasiwasi wowote na kusema kuwa ni kweli kuanzia sasa wana Arusha wamjue kuwa ni shemeji yao yaani Bwashe kwa Mamong'oo wote...
DJ HAAZU
SOMA ZAIDI HABARI ZA ARUSHA CLICK HAPA www.haazu.blogspot.com/

MSIKILIZE SHIJA HAPA CHINI MWENYEWE AKIFUNGUKA MOJA KWA MOJA KWENYE INTERVIEW NA DJ HAAZU NDANI YA MJ FM RADIO ARUSHA

No comments:

Post a Comment