Thursday, February 7, 2013

break news askari wa ulinzi wa kampuni ya securex atekwa na majambazi

Habari kutoka kwa chanzo maalum cha kiitelejensia kimetanabaisha blog hii kuwa askari wa kampuni ya ulinzi ya securex  ametekwa na majambazi yapatayo saba kwa kumfunga mikono na miguu kisha kuvunja na kupora katika duka.

aidha mlinzi huyo majina Ibrahim Kuta amekutwa amefungwa mikono na miguu na mdomoni kuwekewa vitambaa ili asiweze kuongea.
tukio hilo limetokea majira ya saa saba za usiku na duka hilo liko karibu na tawi la diamond trust bank liliopo maeneo ya slipway dtb Masaki  .

kwa mujibu wa mlinzi huyo anasema walikuwa walinzi wanne lakini mpaka sasa hajui wenzake walipo  ambao ni ,Bushiri Omary ,Sadisius Elias na Dominiki ambapo yeye alifungwa kwa kamba na kufunikwa gubigubi.

akimalizia kuelezea tukio hilo mlinzi huyo anasema majambazi hayo takribani saba  yalikuwa na bunduki aina ya bastola na mpaka sasa hajajua ni vifaa au vitu gani vimeibiwa  kutoka katika  duka hilo  la  kubadilisha fedha .

No comments:

Post a Comment