Friday, February 1, 2013
JIJI LA ARUSHA LAZINDUA KAMPENI YA USAFI LEO SHERIA KALI ZAWEKWA
MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ameseama wamepiga hatua kubwa ya
usafi wa jiji la Arusha,na kuwataka wadau mbali mbali wa mazingira
kutoka mkoa wa Arusha kutoa ushirikiano katiak suala la usafi na
kuagiza halmashauri kuunda vijana watakao linda usafi wa jiji hilo
kwa wale watakao kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira.
Mulongo alitoa kauli hiyo jana wakati akiwa amewaongoza viongozi wa
halmashauri na wadau mbali mbali wa utunzaji wa mazingira katika siku
ya uzinduzi wa usafi wa mazingira katika jiji la Arusha , na kuagiza
uongozi wa manispaa kuzingatia usafi wa jiji hilo unapewa kipaumbele
kwa kushirikiana na wananchi .
Alisema pamoja na juhudi zinazofanywa na manispaa kulinda usafi wa
jiji hilo,ni jukumu la kila mwananchi kumlinda mwenzake katika suala
la usafi na kusema wale wote watakao bainika kuchafua mazingira
watatozwa shilingi Elfu 60,000 ambapo kiasi cha shilingi Elfu 20,000
kitachukuliwa na mtu amabaye atamkamata mchafuzi wa mazingira.
Hata hivyo aliseama kuwa ameagiza jeshi la polisi mkoani hapa kuunda
dawati la safi katiak kulinda usafi wa jiji,ili kwa wale waliopewa
dhamana ya kusimamia suala hilo waweze kufanya kazi kwa ufanisi na si
vinginevyo,kwani wasipotimiza wajibu wao watakuwa hawana faida ya
kuwa katika sehemu hizo.
“Mkuu wa Wilaya kama hawa watu watakuwa hawafanyi kazi kwa ufanisi
uwatimue wawekwe watu walio wawajibikaji katiaka meneo yao ya
kazi”alisema Mulongo
Pamoja na mambo mengine amemwagiza Mkurugenzi wa manispaa kuwa
asimamie watu waliopewa zabuni ya kusimamia usafi,vifaa
vinavyohitajika katika kuwekea taka viwekwe,na kamati zote
zinazohusika na jambo hilo zihakikishe vinatimiza wajibu wao.
“Nasema hivi mimi nawashukuru wananchi na wadau m,liojitokeza
kushiriki katika suala hili,lakini mkurugenzi uhakikishe maagizo
niliyoyatoa leo yafuatwe na suala hili la usafi litakuwa ni mwendelezo
kwa kila Ijumaa ya tatu ya mweziƔlisema Mulongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment