Maelfu
ya waumini waliokuwa wamekusanyika katika viunga vya Kanisa la
Mtakatifu Peter Basilica, walipiga kelele za furaha zilizoambatana na
dua za kumshukuru Mungu, baada ya kuona moshi mweupe ukianza kusambaa
katika anga la eneo hilo toka katika jumba ambako Makadinali 115
walikuwa wamejifungia kwa ajili ya kuendesha zoezi la kumchagua kiongozi
mkuu mpya wa Kanira Katoliki duniani.
Na kelele hizo ziliongezeka maradufu
zikiambatana na vigelegele vya shangwe na nderemo, pale Karinali Jorge
Mario Bergoglio, raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 76,
alipojitokeza katika lango kuu la nyumba walikokuwa wamejifungia, huku
akipunga mikono ya furaha yenye kuashiria mwanga mpya kwa waumini wa
kanisa katoli kote duniani.
Kuna mambo mawili ambayo yameleta
msisimko mkubwa katika uteuzi huu. La kwanza likiwa ni lile la
Waitaliano ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kurejea katika
kushikilia wadhifa huo kuukosa tena kwa mara ya tatu, na la pili likiwa
ni ukweli kuwa, hii ni kwa mara ya kwanza kwa Papa kutoka katika nchi
zinazoitwa za ulimwengu wa tatu.
Karinali Jorge Mario Bergoglio, amechagua kuwa aitwe Papa Francis wa kwanza.
No comments:
Post a Comment