|
Mwii wa marehemu Bob Sambeke ukiwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi |
|
Jeneza la marehemu Bob Sambeke likwa nje tayari kwa ajili ya kuaga mwli |
|
Mtoto wa marehemu Jamal akifungua jeneza la marehemu baba yake Bob |
|
Jamal akiwa ameshafunua jeneza la baba yake |
|
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho |
|
Watoto wa marehemu Sia na Getrude |
|
Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani hapo |
|
Watu wakibadilishana mawazo kwa huzuni |
|
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi kuzika |
|
Gari liliokuwa limebeba mwili wa marehemu Bob |
|
Baadhi ya waombolezaji na magari eneo la tukio nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha |
Umati mkubwa wa watu ulifurika nyumbani kwa marehemu “Babu Sambeke” eneo la njiro jijini Arusha kuuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi .
Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka Arusha na Moshi wakionekana kutawala msiba huo.
Magari ya kifahari nayo yalitawala na kusababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Njiro.
Shughuli hizo zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya maziko.
Katika zoezi hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu .
Ndani ya jeneza marehemu alivishwa nguo zake za urubani.
Tofauti na ilivyozoeleka katika misiba mingine hapa nchini, katika msiba huu watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia wenyewe, vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi kinywaji hicho.
Marehemu ameacha watoto watatu ambao ni Sia, Jamal na Getruda.
News Source: Wavuti
No comments:
Post a Comment