Msanii
mahiri wa mziki wa kizazi kipya,Profesa Jay akiwapagawisha mashabiki
waliofurika katika Tamasha la wazi la Vodacom, lililofanyika katika
Ufukwe wa bahari ya hindi Coco Beach, jijini Dar es
Salaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki,waliokwenda kujionea burudani
hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma
mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya Fid Q,akiandaa muziki katika kompyuta
yake ndogo (lap top) wakatiwa Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania,
lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es
Salaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani
ambapo pia walitumia fursa hiyo kwakuelimishwa juu ya huduma mbalimbali
zinazotelewa na mtandao wa Vodacom,wanaoshuhudia kutoka kulia ni Msanii
machachari Dar Stamina na Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom
Tanzania,Ibrahim Kaude.
Umati
wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakipagawa na muziki wakati wa
Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco
Beach, jijini Dar es Salaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki,
waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa
kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Samsung wakiwa tayari kwa kutoa huduma mbalimbali
zilizokuwa zikipatikana ikiwemo na uuzaji wa simu za bei rahisi za Tsh
70,000 na 100,000 ikiwani sehemu ya ofa ya Tamasha la wazi la Vodacom
Tanzania, lililofanyika katika Ufukwewa Coco Beach, jijini Dar es
Salaam.
Msanii
wa Hip Pop nchini mzee wa michano Fid Q akichana vilivyo wakati wa
Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco
Beach, jijini Dar es Salaam.
Msanii
nguli wa muziki wakizazi kipya nchini,Joseph Haule maarufu kama Profesa
Jay akipanda jukwani tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake kwenye
Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwewa Coco
Beach, jijini Dar es Salaam.
Msanii
mahiri wa Hip Pop nchini Fid Q a.k.a Ngosha akiingia katika steji
wakati wa Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika
Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa kizazi kipya wa muziki wa Hip Pop nchini,Dar Stamina akiwapagawisha
mashabiki walio furika katika ufukwe wa CoCo Beach katika Tamasha la
wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika jana katika Ufukwe huo, jijini
Dar esSalaam.
Baadhi
ya mashabiki wakifuatilia jinsi wanamuziki walivyokuwa wanachana katika
Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika jana katika Ufukwewa
Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
MKALI
wamuziki wa Hip Hop nchini, Joseph Haule, maarufu kama Profesa Jay, juzi
alifanya makubwa katika tamasha la wazi lililoandaliwa na Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania nakufanyika katika Ufukwe wa Coco Beach.
Mbali
na Jay, wengine waliokuwapo na kufanya makubwa katika tamasha hilo
lililohudhuriwa na watu wengi, alikuwapo Dar Stamina na Fid Q, ambapo
wote kwa pamoja walifanikiwa kuwapatia burudani za aina yake.
Tamasha
hilo lililofanyika maalum katika Sikukuu ya Pasaka, liliandaliwa maalum
kwa ajili ya kusherehekea na wateja wao, pamoja na kuelimishwa kuhusu
huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya hiyo, ikiwapo Cheka Nao na
promosheni ya Mahela, inayowawezesha wateja kujishindia pesa taslimu.
Akizungumza
katika tamasha hilo, AfisaUdhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania,
Ibrahim Kaude, aliwashukuru Watanzania kwenda kwa wingi katika tamasha
hilo la bure na kushiriki pamoja katika tukio hilo la kiburudani.
Alisema
kuwa katika tamasha hilo, wateja wao walikuwa wakipewa elimu jinsi
mtandao wao unavyofanyakazi, ikiwapo kujulishwa kwa huduma mbalimbali
zinazotolewa na kampuni hiyo kwa kupitia tukio hilo lililofurika watu
wengi.
"Sisi
kama Vodacom tunashukuru kuwa pamoja na mashabiki wa muziki katika tukio
hili la wazi lililoandaliwa mahususi kwa ajili yao, huku tukiamini kuwa
tutaendelea kuwa pamoja kwa huduma mbalimbali zinazotolewa.
"Tunawaahidi
kufanya kazi kwa moyo, pamoja na kuendeleza promosheni zenye mguso wa
aina yake, ikiwapo hii ya Vodacom Mahela, ambapo wateja wetu wanapata
fursa ya kujishindia fedha taslimu kutoka kwetu," alisema Kaude.
Aidha,
msanii Profesa Jay alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani kuwapatia
burudani mashabiki wake na kuungwa mkono, sambamba na kuwaimbisha kila
wimbo aliotaka kuimba katika tamasha hilo lililokuwa na mvuto wa aina
yake.
Baada
ya kushuka kwa msanii huyo, alitoa fursa ya Stamina kupanda, huku dakika
kumi baadaye, Fid Q naye alipanda na kufanya shoo pamoja na mkali huyo
wa Hip Hop anayekubalika na watu wengi kutokana na nyimbo zake kali,
ukiwapo wa 'Kabwela'.
Tamasha
la wazi la Vodacom lililofanyika kwa siku mbili katika ufukwe huo wa
Coco Beach, ambapo wateja wao wote walipata fursa ya kushuhudia burudani
hiyo bila kutoa kiingilio cha aina yoyote.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment