Monday, April 29, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



0 f4c89
Katika mwaka huu 2013, Inatimia  miaka 13 tangu nianze kazi  ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea  kusaidi muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyo shiriki ki kamilifu  kukuza na kulinda sanaa   ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa  sherehe kubwa   na nzuri  ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki.
Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady Jay Dee katika muziki ita ambatana na uzinduzi wa album yangu ya  sita inayo kwenda   kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla   ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora zaJayDee nikishirikiana na  baadhi  y awasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaatarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Munguawabariki

No comments:

Post a Comment