Monday, May 20, 2013

WAPIGA BEDE MARUFUKU KUONEKANA KATIKA KITUO CHA MABASI UBUNGO NA MMILIKI WA MABASI ANAYEMTUMIA MPIGA DEBE KUPATA WATEJA KUCHUKULIWA HATUA KALI YA KISHERIA

Chama cha wamiliki wa  mabasi TABOA,Wakishirikiana na Halamashauri ya Jiji la Dar es salaam
,Jeshi la Polisi  na Sumatra kwa pamoja  wamefikia azimio la  kutokomeza  Tatizo la wapiga debe katika  kituo kikuu  cha mabasi yaendayo mikoani maarufu kama  Ubungo  terminal.

kikao hicho kilifunguliwa rasmi na  mkurugenzi mpya wa  halmashauri ya jiji   Bwana  Mbonea kabwe ,kimefikia na kuamua kufuatilia kwa makini maazimio matatu  muhimu ili kutokomeza tatizo hilo.

Azimio la kwanza  ni kuhakikisha suala la wapiga debe  linaisha  kuanzia sasa kwa mabasi yote  ya abiria kwa magari yenye abiria kuanzia 15,azimio la pili  linawahusu zaidi askari wa jiji ambapo kikao hicho kimefikia uamuzi wa kuongeza  askari hao wa jiji na pia kuhakikisha kuwa askari hao wanakuwepo katika maeneo yao ya kazi kwa kipindi chote kama inavyotakiwa  kwa masaa yote 24.

Azimio la tatu linahusu pande zote yaani halmashauri ya jiji,sumatra,jeshi la polisi na wamiliki wa mabasi kuwa  walinzi baina yao ili kuhakikisha  maazimio hayo matatu yanafuatwa  na endapo  upande mmoja utakiuka na kuvunja  maazimio hayo basi watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Pamoja na maazimio hayo , kikao hicho kimeomba halmashauri ya jiji kuwabadilisha askari wa jiji katika eneo la kituo cha mabasi Ubungo , kwani kukaa kwa muda mrefu kwa askari hao kunatoa mwanya kwao kushiriki  vitendo viovu kutokana na  kuzoea mazingira.

Aidha wamebainisha sababu zinazosababisha  kuwepo au kuendelea kuwepo kwa wapiga debe katika eneo la  Ubungo kuwa ni kutokana na baadhi ya makampuni ya mabasi kuwa na huduma mbovu sasa ili waweze kupata wateja wanawatumia wapiga debe ili kuwavutia wateja.

Meneja wa halmashauri ya jiji anayesimamia kituo cha mabasi Ubungo  ameomba muda ili afanyie kazi maadhimio hayo matatu na kuhakikisha kuwa tatizo la wapiga debe  linaisha kwa haraka  katika kituo cha ubungo na Tanzania kwa ujumla.

Suala la kupambana na wapiga bede  katika eneo la Ubungo limekuja mara baada ya kukithiri kwa vitendo viovu vya utapeli,uizi ,uuzaji wa madaya ya kulevya kama mihadarati, na bangi  pia udanganyifu wa bei za nauli ambapo  tatizo hili limekuwa sugu na kero kubwa kwa watumiaji wa huduma ya usafiri  hasa wageni wanaoingia na kutoka katika kituo hicho cha mabasi cha Ubungo terminal.

Ombi la kufanyiwa kazi kwa maazimio lipo mikononi mwa halmashauri ya jiji na blog hii  ya         G SAMBWETI  iko na wewe bega kwa bega  kufuatilia kinaga ubaga  na kujua  kama kweli maazimio hayo yamefanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment