WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa wanafanyiwa utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana.
Awali watuhumiwa walisomewa mashitaka matatu huku mbunge
akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.
akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana unafanyika mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Godfrey Isaya.
Mashitaka waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo ni kushawishi kufanya vurugu, huku wengine wote makosa yao yakiwa ni kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni kufanya vurugu.
Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi
Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi wengine wa chadema mahakamani hapo huku wafuasi wao wakizuiwa nje ya mahakama
Wafuasi wa Chadema wakiwa wamezuiliwa nje ya viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa wakati mbunge alipofikishwa katika mahakamani mchana huu
Ulinzi mkali kweli kweli
CHANZO : THE CHOICETZ.COM
No comments:
Post a Comment