Saturday, May 18, 2013

JESHI LA POLISI LAKAMATA WATU WATANO NA MILIPUKO MBALI MBALI HATARISHI

Jeshi la polis kanda maalum  Dar es salaam limefanikiwa kukamata watu  5 wakiwa na milipiko hatari, katika msako mkali unaendelea jijini  Dar es salaam ,msako huo amboa umefanyika katika maeneo ya kunduchi  na watuhumiwa  waliokamamtwa ni :JUMA KHALIFANI miaka  24,makazi wa kunduchi mtongani,Ruben Patric  miaka 26 mkazi wa kunduchi mtongani,Happy Charles miaka  28 mkazi wa Kunduchi mtongani ,Sadick Seif miaka 32 na mkazi wa kunduchi mtongani na  Idd Shaban  miaka 40 mkazi wa  kunduchi mtongani.

Kukamamtwa kwa watuhumiwa hawa kumetokana na jitihada mathubutu baina ya wasamasiria wema na Jeshi la polisi na milipuko iliyokammatwa ni pamoja na a nyaya 62 za mlipuko zikiwa zimeunganishwa na betri,vifaa ya kusababisha mlipuko (supreme plain denonator no.8) nyaya ndefu  mizunguko minne ,tube 20 za urefu cm 30  zilizojazwa mbolea ya urea  na tambi 1.

Vifaa vyote hivyo hapo juu ni hatari vikiunganishwa na vinawezaa kuhatarisha maisha ya  watu na uharibifu wa mali,aidha milipoko hiyo  pia inatumika katika  kupasulia miamba,hivyo uchunguzi  unafanyika zaidi ili kubain  na kujua madhumuni halisi ya  watuhumiwa hawa kumiliki vifaa saidizi vya milipuko hiyo hatari.


 ukamataji wa milipuko hiyo ulitokana na  operesheni maalum inayoendelea jijni Dar es salaam, Opereshen hiyo ilifanikisha  kukamata  dawa za kulevya  aina  ya Bangi  gunia moja,katika  operesheni  hiyo gari namba T 772 BYC aina ya Noah rangi ya fedha pamoja na  bajaji miguu mitatu no T 959 BTE rangi ya  blue  nazo zimekamatwa  zikiwa  nyumbani  kwa mtuhumiwa  SADICK SEIF ambaye  alishindwa  kuthibitisha  kuhusu uhalali wa  kumiliki  gari hilo na pikipiki hiyo ,hivyo atapelekwa mahakamani  baada ya upepelezi kukamilika.

kamanda Suleimani Kova kwa niaba ya jeshi la polisi anawashukuru wananchi kwa wema wa kutoa taarifa hizo na kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa

No comments:

Post a Comment