Saturday, May 18, 2013

LEO PATASHIKA NGUO KUCHANIKA UWANJA WA TAIFA MECHI KATI YA WATANI WA JADI

Jeshi la polisi kanda maalum Dar es salaam kwa kushirikiana na  na vyombo vingine vya  ulinzi na usalama   limejiandaa  kuhakikisha  mchezo wa leo wa Simba na Yanga .

Jeshi la polisi limeomba wananchi wasiwe na shaka lololte  la kiusalama na  pia watuwape ushirikiano  kwa kutoa taarif a  kwa jambo lolote lile  watakaloona  kuwa  linaweza  kuwa chanzo cha  kuvunja amani  kwa kipindi chote  watakapokuwa ndani au nje ya uwanaja.

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama  vitafanyaia kazi  taarifa hizo haraka  na kuwachukulia  hatua watuhumiwa  wa tukio  husika  kulingana na  sheria za nchi /kanuni  za usalama na shirikisho la  soka duniani ( FIFA SAFETY GUIDELINE)

Vilevile  kamanda kova amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuzingalia  timu  za Simba na Yanga  na  wahakikishe  wanatumia miuondombinu  ya uwanja  kwa usalama na amani kwani  uwanja  huo  nikitega  uchumi kikubwa ambacho serikali imejenga kwa manufaa ya watanzania wote.

Pamoja na kuimarisha  ulinzi wa ndani  na nje  ya uwanja (inner and outer  perimeter security measues), kwa  kipindi cha mechi hizi  watatumia camera  za CCTV ili kufuatilia  mwenendo wa  matukio yote  itakuwa ni mara ya pili kwa camera hizo kutumika ,mara ya kwanza  zilitumika mwaka 2007  wakati wa ufunguzi wa uwanja.

hivyo wananchi wakumbuke kuwa matukio  yote zitahifadhiwa  na  kutumika  katika kubaini mtu yeyote atakayeonekana amefanya uvunjifu wa sheria.

ifuatayo ni moja ya ya mikakati ya kuimarisha usalama watakayotekeleza:
1.ulinzi wa uwanja.

.jeshi la polisi halitaruhusu mikisanyiko isiyo na lazima maeneo yote  ya nje ya uwanja hasa  kuanzia  eneo la msikitini  hadi maeneo la baaa ya minazini
pia magari hayatarusiwa  kuegeshwa  katika  eneo hilo  na badala yake  kwa wataopenda kwenda na magari yao ,watafute maeneo mengine salama   yakuegesha magari hayo  ikiwezekana wapaki pembezoni mwa barabara ya  kuegesha magari yao kuanzia eneo la  kijiji cha ichezo hadi uwanja wa uhuru.


.Baada  ya michezo  askari wataendelea kufanya patrol katika barabara zote na njia  za mitaa ya karibu na uwanja  wa taifa  ili kuzuia uwezekano wa vibaka kupora watu.

2.MIKAKATI YA KUPUNGUZA FOLENI YA MAGARI WAKATI WA KUINGIA UWANAJANI 

.kwa kipindi kirefu  tunakuwa na  michezo  mikubwa  barabara ya  UWANJA WA UHURU HADI KONA Y DUCE/KEKO inakuwa  na msongamano  mkubwa .hivyo ,barabara hiyo itafungwa  na m agari  yote yatapita Mandela Road.

.Sambamba nakufungwa barabara hiyo hakutakuwa na maegesho ya magari  katika eneo la parking la uwanja  waTaifa.Magari yatakayoruhusiwa  kuingia katika eneo maalum  la parking ya uwanja ni:

-magari ya vyombo  vya ulinzi  na usalama
-magari ya timu zinazocheza na viongozi watimu
-magari ya watendaji mbali mbali
-magari ya viongozi wakuu wa serikali  na TFF/ZFF

KUMBUKA
Maeneo tajwa yatakuwa na askari wa kutoshha kuhakikisha  mikakati  hiyo kiusalama  inatekelezwa
3.ULINZI KATIKA MILANGO YA KUINGIA UWANJANI
4.uthibiti wa uhujumu wa mapato
5.ulinzi wa majukwaa
5.ulinzi katika majukwaa
6.ulinzi ndani ya uzio
7.Msisitizo  wa matumizi ya Tahema.

.kwa kuwa uwanja wetu ni wa kisasa na una camera za CCTV  jeshi la polisi litatumia camera hizo kufuatilia matukio  yote  ndani na nje  ya uwanja,kumbumbuku  za matukio maovu  zitatumika  kuwabain wahusika  na kuwachulia  hatua kwa mujibu wa sheria.

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi  na usalama  linaomba ushirikiano  wa kutosha kwa wananchi ,mashabiki watimu  zinazocheza  na wadau wote , kwa kuunganisha nguvu za pamoja na mchezo huo uchezwa na kumalizika kwa usalama.

MWISHO :JESHI LA  POLISI LINATOA  WITO KWA WALE WOTE AMBAO WATAVUNJA SHERIA  HATAUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.


No comments:

Post a Comment