Katika mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini , Kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani pamoja na utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke , jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 4 na 5 mwenzi May 2013.
Tamasha la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi, Madii akiwa na kundi zima la tiptop connection, pamoja na wakali wa hipop Fid Q , Roma Mkatoliki na Ney wa mitego .
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando amesema, tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo Airtel yatosha na kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano bora na bei nafuu wa Airtel.
Na mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es salaamawa na kuwapa nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya Airtel yatosha, Airtel Money na internet ya kasi ya 3.75G, kupata elimu kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na mtandao wa Airtel kwa wale wateja wapya.
Kiingilio ni BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu na kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza Mmbando.
Kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.
No comments:
Post a Comment