Hatimaye mkutano wa siku mbili wa
shirikisho la wanasheria wakuu wa nchi za Africa mashariki leo umefika tamati .
Mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana katika ukumbi wa hotel ya serena
jijini dar es salaam leo
umehitimishwa na rais wa shirikisho hilo
na mwanasheria mkuu wa watu wa kidemokrasia wa watu wa Rwanda bwana Martin Ngonga.
Katika kuhitimisha mkutano huo raisi wa
shirikisho hilo bwana martini ngoga aliweza kuongelea yale yaliyojadiliwa katika
mkutano huo kuwa ni uanachama wa wanasheria ,raslimali watu,pia ameweza
kuongelea juu ya fursa waliyopata ya kubadilishana uzoefu kutoka kwa wanasheria
kutoka nchi mbali mbali za shirikisho
hilo la Africa mashariki na mafanikio waliyopata kwa kuzuia na kukomesha uhalifu wa ndani na nje ya nchi.
Nae makamu wa raisi wa shirikisho la
wanasheria na mwanasheria mkuu wa Tanzania bwana Eliaza feleshi ameweza kueleza
sababu au changamoto zinazokabili
mahakama na vyombo vya sheria katika kutoa haki kwa jamii kuwa ni
ushirikiano mdogo kutoka kwa jamii katika kutoa vielelezo au vidhibitisho
katika kesi mbali mbali kutokana na wahalifu wengi kuwa miongoni wa jamii zetu
zinazotuzunguka
mwisho aliomba jamii kutoa ushirikiano kwa
vyombo vya sheria ili kutoa fursha kwa vyombo vya sheria kupata vithitisho na kuweza kutoa hukumu
sitahiki kwa walengwa wa makosa mbali
mbali ndani na nje ya Tanzania.
Swali kwa kwako Mtanzania mwenzangu je? ni wahalifu wangapi unawajua wanatafutwa na vyombo vya sheria na bado hujatoa taarifa kwa vyombo husika
No comments:
Post a Comment