Katika maandalizi ya kuadhimisha siku ya
wauguzi duniani yatakayofanyika
tarehe 12 mwezi wa 5 mwaka huu,chama cha
wauguzi Tanzania Tanna wamejiandaa kutoa huduma kwa jamii kuanzia kesho katika
viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha dar es salaam
siku ya maadhimisho hayo mgeni rasm atakuwa
meya wa jiji la dar es salaam pamoja wageni wengine mbali mbali kama
mkurugenzi wa jiji,muuguzi mkuu wa jiji ,mkuu wa chuo kikuu cha dar es salaam
na waganga wakuu wote wa hospitali za serikali na hospitali binafsi.
huduma watakazo toa ni pamoja na kutoa ushauri
na kupima kwa hiari,kutoa damu salama,elimu kuhusu magongwa yasiyo
ambukiza,elimu ya uzazi wa mpango ,uchunguzi wa
kansa ya kizazi,huduma ya magonjwa ya akili ,elimu kuhusu ujasiria
mali na elimu juu ya tuko wangapi
lengo kuu la kufanyika kwa shughuli hii ni
kutimiza malengo ya milenia ambayo
ni kuondoa umasikin na njaa,kupunguza
vifo vya watoto,kuboresha afya za wamama
wenye umri wa kuzaa ili kupunguza vifo
pamoja na kupunguza maabukizi ya virusi
vya ukimwi yaani VVU.
mwisho mwenyekiti wa Tanna bi Niwabigiry
alimazia kwa kusema changamoto kubwa inayokabili ni upungufu mkubwa wa wauguzi
na upungufu wa vitendea kazi
No comments:
Post a Comment