Wednesday, May 1, 2013

UTALII WA KITAMADUNI NI SULUHISHO LA AJIRA-JAMBO FESTIVAL




MKURUGENZI WA JAMBO FESTIVAL AUGUSTINE MICHAEL
Serikali imeaswa kuwekeza katika utalii utokanao na vivutio vya Kijamii hasa maisha ya watu na vinavyowazunguka badala ya kuangalia kwa nguvu kubwa upande mmoja tu wa mbuga na  mali asili.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi inayosimamia na kuhamasisha uhifadhi wa maisha ya kitamaduni pamoja na sanaa kwa ujumla wake yaani Jambo Festival Bwana Augustine Michael Namfua wakati akitoa tuzo maalum za kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja au nyingine walifanikisha tamasha la JAMBO FESTIVAL mwaka 2012.
Amesema kuwa Watanzania  wana kila sababu ya kunufaika na maisha yao ya asili kwa vile ndani yake kumekuwa na maadili, miiko , kuheshimiana, kushirikiana sambamba na kuonyesha vipaji kwa kutengeneza kazi za sanaa kama uhunzi, uchongaji wa vinyago, ususi, uchoraji, uimbaji, uchezaji ngoma, ufinyanzi, utungaji, ufumaji, tiba za asili, uandaaji wa vyakula vya asili n.k. 

Bwana Augustine ameongeza kuwa kwa sasa taifa linapoteza pato kubwa kwa vile sanaa imekuwa kama vile jambo la ziada lisilo na maana wakati jamii kubwa hasa vijana wakibaki mitaani wakiwa wamebeba lawama kwa serikali.
Katika utoaji wa tuzo hizo ambao umefanyika katika hotel yenye historia na heshima kubwa  jijini Arusha yaani Arusha hotel ambayo ilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na wakoloni katika eneo ambalo ni katikati ya Afrika , ilitoa nafasi kwa wadau kadhaa ikiwemo kampuni ya Mega Trade Investment chini ya kinywaji chao cha K-Vant Gin kuchukua tuzo ya juu ya wadau waliojotoa kwa karibu zaidi. 

Hata hivyo kwa upande wa Wasanii walikuwa wameshiriki katika tamasha hilo kwa Mwaka jana Worrios From The East pamoja na S.U.A nao pia walipata tuzo Maalum kwa ushiriki wao.

HATA HIVYO ALIITAJA TAREHE MAALUM YA JAMBO FESTIVAL KWA MWAKA HUU WA 2013 KUWA NI KUANZIA TAREHE 23 HADI 27 OCTOBER 2013

HAWA NI BAADHI YA WALIOPATA TUZO
Afisa Habari Manispaa Ya Arusha Integenjwa Hosea
  
Diwani wa Moshono Paul Mapsen akipokea Tuzo ya Meya wa jiji la Arusha

Mkuu wa Masoko MEGA Trade Gudluck Kway

MC alikuwa Huyu Baraka Sunga Mhariri Mkuu Sunrise Radio

BlackGizaz Wa Warrious From The East akipokea Cheti

Mwakilishi wa Sun Bright Hotel

Mkurugenzi wa Ufundi Sunrise Radio Dionice Moyo akipokea Tuzo ya Radio

Mwakilishi wa

Mwakilishi wa Tingatinga Arts Group

Kulia ni Producer Daz Nalage Na Baadhi ya Wasanii wa S.U.A

Gael Mkurugenzi wa Alliance France
Mwakilishi wa Arusha

habari kwa hisani ya http://haazu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment