Baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakiwa katika foleni wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi, ambapo katika Sherehe hizo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidick, huku sherehe hizo kitaifa zikifanyika Kitaifa Mkoani Mbeya, na Mgeni Rasmi huko ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wengine wakati wakisimama kupokea maandamano hayo.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, wakipita mbele ya jukwaa kuu na maandamano na mbwembwe za kucheza Kiduku, wakati wa sherehe hizo.
Wafanyakazi wa TALGWU, wakipita mbele ya jukwaa kuu na Bango lenye ujumbe.
Twiga Cement wao walikuwa wakipromoti bidhaa yao tu bila hata bango lenye ujumbe kuhusiana na sherehe hizo.
Maandamano yakiendelea kupita mbele ya jukwaa kuu.
Maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu........
'Watenda Haki' wakipita na bango lao mbele ya jukwaa kuu......SOURCE:SUFIANMAFOTO BLOG
habari na mhariri mkuu wa G SAMBWETI
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Sadik
Meck Sadik amewaongoza leo wafanyakazi
wa vyama mbali mbali vya jiji la Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya
wafanyakazi duniani na kauli mbiu ha mwaka huu ikiwa ni KATIBA MPYA IZINGATIE
USAWA NA HAKI KWA TABAKA LA WAFANYAKAZI; na wafanyakazi wapatao 24 walitunukiwa
zawadi za ufanakazi bora mwaka huu.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa jiji
la Dar es salaam yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoji huku kitaifa
ikifanyik mkoani mbeya na mgeni rasmi akiwa ni rais wa jamhuri yaMuungano dk
Jakaya Mrisho kikwete.
katika siku ya leo wafanyakazi kutoka vyama
mbali mbali wameitikia wito wa kuhudhuria na
kusababisha uwanja wa mnazi mmoja kufurika watu na kusababisha magari kutoka makampuni mbali mbali kukosa
sehemu ya maegesho ya kuonyesha kazi zao .
Katika
risala iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi mh Sadik meck sadik ,
kuliorodheshwa changamoto mbali mbali zinazowakabili wafanyakazi mojawapo
likiwa ni tatizo la ongezeko la nauli,tatizo la makato kutofautiana baina ya vyama na vyama,tatizo
la kuchelewa kupelekwa kwa makato ya mfanyakazi.
Mwisho risali ilimaliziwa kwa kutoa ombi
kwa serikali kukomesha tabia ya waajiri
wa sekta binafsi kuwafanyisha kazi kwa muda mrefu wazawa huko wafanyaka kutoka
nje wakifanya kazi ambazo ni za muda
mfupi kwa mishahara minono ,kazi ambaZo hata watanzania wanaziweza.
Nae Mgeni rasmi katika kujibu risala hiyo ya wafanyakazi
amewahakikishia kuwa mwakani watatumia uwanja wa uhuru ili kuepuka msongamano ,
pia aliweza kuongelea na kuwahoji wakuu wa wilaya kuhusu tatizo la kuchelewa
kupelekwa kwa makato ya wafanyakazi katika mifuko ya pensheni na kuweka tamko kuwa ifikapo juni 30 makato
ya wafanyakazi wote yawe yamepekwa katika mifuko husika ya pensheni.
Na katika suala la kupunguza matatizo ya
msongamano mh Sadik amesema kuwa hadi
kufikia mwezi wa nane mwaka huu watazindua usafiri wa majini kwa kutumia boti
kutoka kivukoni hadi bagamoyo ambapo boti hiyo itasimama katika vituo vinane pia akagusia matarajia ya mabasi makubwa ili kupunguza na kutokomeza suala la foleni na pia kutokomeza tatizo la usafiri ,huku akiwatoa hofu wamiliki wa daladala kuwa watapa vibali vya kufanya kazi katika mikoa mingine yenye uhitaji wa daladala na mwisho
kabisa mgeni rasmi aliwakimbusha wafanyakaji kukumbuka kujikinga na gonjwa
hatari la ukimwi.
No comments:
Post a Comment