Makamu
wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akimvika cheo cha Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP), John Makuli (katikati), baada ya kufuzu
mafunzo hayo. Maofisa 295 walifuzu mafunzo hayo na kutunukiwa vyeo vya
wakaguzi na maofisa. Makamu wa Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye
maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa na ndugu za maofisa waliofuzu mafunzo hayo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Gwaride
maalumu la maofisa hao likipita mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk.
Mohammed Gharib Bilal kwa mwendo wa haraka kwenye hafla ya
kufunga mafunzo ya maofisa na wakaguzi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika
viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
Maofisa wa Polisi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Askari wa Kikosi cha Farasi wakipita katika uwanja wa paredi wakati wa hafla hiyo.
Wahitimu hao wakiwa uwanja wa paredi.
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal akitoka kukagua gwaride la maofisa hao waliohitimu mafunzo ya uofisa na ukaguzi.
Makamu wa Rais akivika mmoja wa Maofisa hao, nishani wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal, akimvika cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi Alikunda Urio.
Waziri
wa M,ambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emanuel Nchimbi (katikati), akiteta
jambo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Hassan
Ndomba (kulia) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Gwaride maalumu la maofisa hao likipita mbele ya mgeni rasmi.
Wahitimu hao wakila kiapo cha utii.
Maofisa wa Polisi wakionesha utalaamu wa kucheza mchezo wa karate wakati wakikabiliana na adui.
Mmoja wa askari wa mwanamke wa jeshi hilo (kulia), akionesha namna ya kukabiliana na adui.
Askari hao wakionesha namna ya kukabiliana na adui kwa kutumia mikono.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
namna ya kukabiliana na wananchi wakati wa vurugu. (Picha zote na habari na www.mwaibale.blogspot.com)
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dk. Mohammed Gharibu Bilal
amesema serikali haitakuwa tayari kuvunja kiapo chake na kuona amani ya
nchi natoweka.
Kauli hiyo
aliitoa wakati akifunga mafunzo ya Uofisa na Wakaguzi Wasaidizi kwenye
Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.
"Serikali
haikotayari kuona amani ya nchi ikivurugwa kupitia kundi la aina fulani
hivyo ninyi polisi ndio wenye wajibu wa kulinda amani hiyo pamoja na
watu na mali zao" alisema Bilal.
Dk.Ghalib
Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo alisema
hivi sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na matukio ya vurugu
zinazotokana na vyanzo mbalimbali.
Alisema
baadhi ya vurugu hizo zinasababshwa na hisia za kiimani,kisiasa na
kijiografia ambazo madhara yake ni makubwa na tayari yameathiri wananchi
wengi.
"Wananchi
wa Tanzania hawapendi kabisa kuona nchi hii ikigeuka kuwa ukanda wa
vurugu, tena sisi kama Taifa hatuwezi kunifaika na vurugu
zisizoisha"alisema Dk.Bilal
Alisema
jeshi la polisi lilihapa na kusimamia amani na utulivu nchini hivyo
tunaamini kuwa amani hiyo italindwa kutokana na viapo walivyoapa.
Aliongeza
kuwa hivi karibuni kumeibuka baadhi ya wananchi kwa sababu zao wameanza
kubeza na kudharau kazi wanazofanya askari wetu kibaya zaidi watu hawa
wanaota siku moja watashika dola ya nchi yetu ili waiongoze nchi.
"Siamini
macho yangu kama ndoto zao zitatimia kama wataendelea na tabia hii ya
kudharau na kutoeshimu mamlaka tulizojiwekea wenyewe kwani kazi ya
askari si sawa na kufanya siasa kwani kazi ngumu lakini ni muhimu
kuliwekea Taifa katika twasira ya maendeleo"alisema Bilali.
Wakati
huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.Emanuel Nchimbi amesema
askari wa tano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini wanatarajiwa
kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya kuiba nyaraka mbalimbali za serikali
na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha baada ya kufungua akaunti kwa
kutumia jina la jeshi hilo.
Alisema
watu hao tayari wameshakamatwa na muda wowote watafikishwa Mahakamani
kujibu tuhuma zao kwa kuwa tayari jalada lao limeshapelekwa kwa
Mwanasheria wa Serikali.
Nchimbi
alisema kutokana na tuhuma hizo kujitokeza aliamua kuunda tume ya
uchunguzi ili kugundua ni nani anayefanya tuhuma hizo, tume hiyo ilikuwa
inaongozwa na Kamishna Msaidizi wa polisi Advocate Nyombi kutoka makao
makuu ya upepelezi ya makosa ya jinai.
"Sikutaka
kufumbia macho suala hilo timu hiyo ilifanya kazi yake na juni 22 mwaka
huu ilitoa majibu na kubaini askari wa zimamoto wenyewe ndio wanahusika
na ubadhilifu ndani ya jeshi la zimamoto nchini"alisema Nchimbi.
Aliwataja
watuhumiwa wanaotuhumiwa kuwa ni Mkaguzi Msaidizi wa zimamoto Joseph
Mwasabeja, Koplo wa zima moto Hashimu Kapamba, Koplo wa zimamoto
Boniface Mbele,Sajini Meja wa Zimamoto Dankan Mwakajinga na Koplo wa
Zimamoto Kenned Kipali ambao wanatoka ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na
nje ya mkoa.
Hata hivyo
Waziri Nchimbi alisema vitu walivyopatikana navyo ni pamoja na hati ya
akaunti ya benki inayotumika kuibia serikali,mikanda 82 ya askari wa
jeshi la zimamoto na stakabadhi mbalimbali za malipo zinazotumiwa na
jeshi hilo.
Aidha,
alisema mtuhumiwa Kapamba alikamatwa na na stakabadhi za malipo ya
serikali (ERVs)ambazo ni za kughushi hati na fomu mbalimbali za jeshi
hilo zinatumika katika ukaguzi wa viwanda na majengo.
Vilevile
alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao mtuhumiwa mmoja ni mtoto wa
Kamishina wa pwani,ambaye aliwasiliana naye na kumtaka amwasilishe mtoto
wake ndani ya masaa mawili kwa ajili ya kujieleza dhidi ya tuhuma hizo.
Hivyo
aliwataka maofisa hao wajue kuwa wanakazi kubwa wanapokwenda kazini na
aliwataka wananchi wote watimize wajibu wao kwa kufuata sheria za nchi
na kujiepusha na vitendo vya namna hii ambavyo vinavunja heshima yao na
jeshi la zimamoto.
No comments:
Post a Comment