Naibu Katibu Mkuu wa baraza la Taifa la Mitihani, Dk. Charles E. Msonde akisoma matokeo hayo ya mitihani ya kidato cha sita kwa mitihani iliyofanyika mwaka huu nchini kote.
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) ULIOFANYIKA FEBRUARI 2013
UTANGULIZI
Baraza la Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 94 kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2013liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika tarehe 11 - 27 Februari 2013.
USAJILI NA MAHUDHURIO
Watahiniwa wote
Jumla ya watahiniwa 52,513 waliandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 wakiwemo wasichana 16,934 (32.25%) na wavulana 35,579 (67.75%). Kati ya watahiniwa 52,513waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Februari 2013, watahiniwa 50,611 sawa na asilimia96.38 walifanya mtihani na watahiniwa 1,902 sawa na asilimia 3.62 hawakufanya mtihani.
Watahiniwa wa Shule
Kwa Watahiniwa wa Shule, kati ya watahiniwa 43,231 waliosajiliwa, watahiniwa 42,952 sawa na asilimia 99.35 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa ni 13,883 (99.54%) na wavulana ni29,069 (99.27%). Watahiniwa 279 (0.65%) hawakufanya mtihani.
Watahiniwa wa Kujitegemea
Kwa upande wa Watahiniwa wa Kujitegemea, kati ya watahiniwa 9,282 waliosajiliwa, watahiniwa7,659 sawa na asilimia 82.51 walifanya mtihani na watahiniwa 1,623 sawa na asilimia 17.49hawakufanya mtihani.
MATOKEO YA MTIHANI
Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 44,366 sawa na asilimia 87.85 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 14,622 sawa na asilimia 89.19 wakati wavulana waliofaulu ni 29,744 sawa na asilimia 87.21.
Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.
Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana ni 26,956 sawa na asilimia 93.03.
Mwaka 2012 Watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 4,124 sawa na asilimia 53.87. Mwaka 2012 Watahiniwa wa Kujitegemea 5,883 sawa na asilimia 64.96 walifaulu mtihani huo.
UBORA WA UFAULU
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 35,880 sawa na asilimia 83.74 wamefaulu katika madaraja I - III wakiwemo wasichana 12,108 sawa na asilimia 87.30 na wavulana 23,772 sawa na asilimia 82.04.
Jedwali la 1 linaonesha ufaulu kwa kila Daraja kwa Watahiniwa wa Shule na kwa Jinsi:
Jedwali la 1: Ufaulu wa kila Daraja kwa Watahiniwa Wa Shule
Daraja la Ufaulu
|
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
| |||
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
| |
I
|
188
|
0.65
|
137
|
0.99
|
325
|
0.76
|
II
|
3,142
|
10.84
|
2,230
|
16.08
|
5,372
|
12.54
|
III
|
20,442
|
70.55
|
9,741
|
70.24
|
30,183
|
70.45
|
IV
|
3,184
|
10.99
|
1,178
|
8.49
|
4,362
|
10.18
|
0
|
2,021
|
6.97
|
583
|
4.20
|
2,604
|
6.08
|
UFAULU WA MASOMO KWA WATAHINIWA WA SHULE
Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule unaonesha kwamba kwa masomo ya History,Geography, English Language, Chemistry, Biology, Agriculture, Computer Science,Economics na Accountancy yamefanyika vizuri zaidi ukilinganisha na mwaka 2012.
Jedwali la 2 linaonesha idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu masomo mbalimbali kwa mwaka 2012 na mwaka 2013.
Jedwali la 2: Ulinganifu wa ufaulu kwa masomo kwa mwaka 2013 na 2012
NA.
|
MASOMO
|
WALIOFAULU 2012
|
WALIOFAULU 2013
| ||
IDADI
|
ASILIMIA
|
IDADI
|
ASILIMIA
| ||
111
|
GENERAL STUDIES
|
38,468
|
87.09
|
16,507
|
38.53
|
112
|
HISTORY
|
21,482
|
92.86
|
18,987
|
97.33
|
113
|
GEOGRAPHY
|
21,823
|
92.40
|
20,578
|
96.87
|
121
|
KISWAHILI
|
13,608
|
97.89
|
11,840
|
96.95
|
122
|
ENGLISH LANGUAGE
|
12,903
|
89.50
|
11,081
|
93.61
|
131
|
PHYSICS
|
7,526
|
70.58
|
5,788
|
46.34
|
132
|
CHEMISTRY
|
10,289
|
71.14
|
13,809
|
83.87
|
133
|
BIOLOGY
|
7,338
|
77.90
|
9,181
|
87.05
|
134
|
AGRICULTURE
|
506
|
92.67
|
537
|
98.35
|
136
|
COMPUTER SCIENCE
|
17
|
43.59
|
74
|
80.43
|
142
|
ADVANCED MATHEMATICS
|
7,786
|
84.44
|
6,895
|
69.32
|
151
|
ECONOMICS
|
8,001
|
90.66
|
8,173
|
93.53
|
152
|
COMMERCE
|
1,405
|
90.41
|
1,573
|
88.57
|
153
|
ACCOUNTANCY
|
1,314
|
84.56
|
1,660
|
93.42
|
SHULE ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI
Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) ambapo A = 1,B = 2, C = 3, D = 4, E = 5, S = 6 na F = 7. Shule zimegawanywa katika makundi mawili kulingana na idadi ya watahiniwa kama ifuatavyo:
Zenye watahiniwa 30 na zaidi (Jumla ni 329);
Zenye watahiniwa pungufu ya 30 (Jumla ni 166).
6.1 Shule kumi (10) bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi
NA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MARIAN GIRLS S.S
|
158
|
PWANI
|
2
|
MZUMBE S.S
|
125
|
MOROGORO
|
3
|
FEZA BOYS’ S.S
|
59
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
ILBORU S.S
|
171
|
ARUSHA
|
5
|
KISIMIRI S.S
|
50
|
ARUSHA
|
6
|
ST.MARY'S MAZINDE JUU S.S
|
80
|
TANGA
|
7
|
TABORA GIRLS S.S
|
74
|
TABORA
|
8
|
IGOWOLE S.S
|
58
|
IRINGA
|
9
|
KIBAHA S. S
|
184
|
PWANI
|
10
|
KIFUNGILO GIRLS S.S
|
61
|
TANGA
|
6.2 Shule kumi (10) za Mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi
NA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
PEMBA ISLAMIC COLLEGE
|
67
|
PEMBA
|
2
|
MAZIZINI S.S
|
127
|
UNGUJA
|
3
|
BARIADI S.S
|
34
|
SIMIYU
|
4
|
HAMAMNI S.S
|
174
|
UNGUJA
|
5
|
DUNGA S.S
|
35
|
UNGUJA
|
6
|
LUMUMBA S.S
|
292
|
UNGUJA
|
7
|
OSWARD MANG’OMBE S.S
|
120
|
MARA
|
8
|
GREEN ACRES S.S
|
87
|
DAR ES SALAAM
|
9
|
HIGH VIEW INTERNATIONAL
|
34
|
UNGUJA
|
10
|
MWANAKWEREKWE “C” S.S
|
126
|
UNGUJA
|
6.3 Shule kumi (10) bora katika kundi la shule zenye watahiniwa
chini ya 30
NA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
PALLOTI GIRLS S.S
|
26
|
SINGIDA
|
2
|
ST. JAMES SEMINARY
|
20
|
KILIMANJARO
|
3
|
PARANE S.S
|
12
|
KILIMANJARO
|
4
|
SANGITI S.S
|
12
|
KILIMANJARO
|
5
|
ITAMBA S.S
|
18
|
NJOMBE
|
6
|
MASAMA GIRLS S.S
|
19
|
KILIMANJARO
|
7
|
KIBARA S.S
|
11
|
MARA
|
8
|
ST. LUISE MBINGA GIRLS S.S
|
19
|
RUVUMA
|
9
|
ST. PETER’S SEMINARY
|
17
|
MOROGORO
|
10
|
PERAMIHO GIRLS S.S
|
15
|
RUVUMA
|
6.4 Shule kumi (10) za Mwisho katika kundi la shule zenye
watahiniwa chini ya 30
NA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MBARALI PREPARATORY SCHOOL
|
21
|
UNGUJA
|
2
|
PHILTER FEDERAL S.S
|
23
|
UNGUJA
|
3
|
ST.MARY'S S.S
|
24
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MZIZIMA S.S
|
12
|
DAR ES SALAAM
|
5
|
HIJRA SEMINARY
|
28
|
DODOMA
|
6
|
TWEYAMBE S.S
|
19
|
KAGERA
|
7
|
MPAPA S.S
|
17
|
UNGUJA
|
8
|
AL-FALAAH MUSLIM
|
17
|
UNGUJA
|
9
|
PRESBYTERIAN SEMINARY
|
14
|
MOROGORO
|
10
|
NIANJEMA S.S
|
16
|
PWANI
|
WATAHINIWA WALIOFANYA VIZURI ZAIDI
Watahiniwa waliofanya vizuri zaidi wamepatikana kwa kuangalia GPA kwenye masomo ya “combination” pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata. Masomo ya hiari (optional subjects) hayakujumuishwa katika kuwapanga wanafunzi bora.
Watahiniwa Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Sayansi
NA.
|
JINA
|
JINSI
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ERASMI INYANSE
|
M
|
ILBORU
|
ARUSHA
|
PCM
|
2
|
MAIGE R MAJUTO
|
M
|
KISIMIRI
|
ARUSHA
|
PCM
|
3
|
GASPER SINGFRID MUNG'ONG'O
|
M
|
FEZA BOYS'
|
DAR ES SALAAM
|
PCB
|
4
|
GASPER JAMES SETUS
|
M
|
ST. JAMES SEMINARY
|
KILIMANJARO
|
PCM
|
5
|
LUCYLIGHT E MALLYA
|
F
|
MARIAN GIRLS
|
PWANI
|
PCB
|
Wasichana Watano (05) bora kitaifa kwa Masomo ya Sayansi
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
LUCYLIGHT E MALLYA
|
MARIAN GIRLS
|
PWANI
|
PCB
|
2
|
EDNA BARAKA KIBANGO
|
MSALATO
|
DODOMA
|
PCB
|
3
|
SARAH SEVERIN KIMARIO
|
ST.MARY'S MAZINDE JUU
|
TANGA
|
PCM
|
4
|
VERONICA S MWAMFUPE
|
MARIAN GIRLS
|
PWANI
|
PCM
|
5
|
BEATRICE D ISSARA
|
ST.MARY GORETI
|
KILIMANJARO
|
PCM
|
Wavulana Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Sayansi
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ERASMI INYANSE
|
ILBORU
|
ARUSHA
|
PCM
|
2
|
MAIGE R MAJUTO
|
KISIMIRI
|
ARUSHA
|
PCM
|
3
|
GASPER SINGFRID MUNG'ONG'O
|
FEZA BOYS'
|
DAR ES SALAAM
|
PCB
|
4
|
GASPER JAMES SETUS
|
ST. JAMES SEMINARY
|
KILIMANJARO
|
PCM
|
5
|
CHRISTOPHER L STANSLAUS
|
MZUMBE
|
MOROGORO
|
PCB
|
Watahiniwa Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Biashara
NA.
|
JINA
|
JINSI
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ERIC ROBERT MULOGO
|
M
|
TUSIIME
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
2
|
ALICIA FILBERT
|
F
|
NGANZA
|
MWANZA
|
ECA
|
3
|
EVART EDWARD
|
M
|
KIBAHA
|
PWANI
|
ECA
|
4
|
ANNASTAZIA P RENATUS
|
F
|
TAMBAZA
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
5
|
PETERSON P MEENA
|
M
|
MBEZI BEACH
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
Wasichana Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Biashara
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ALICIA FILBERT
|
NGANZA
|
MWANZA
|
ECA
|
2
|
ANNASTAZIA P RENATUS
|
TAMBAZA
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
3
|
MARY AMOS BUJIKU
|
ST.ANTHONY'S
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
4
|
GETRUDA GHATI PATRICK
|
BARBRO-JOHANSSON
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
5
|
LETICIA PARTSON KAYANGE
|
WERUWERU
|
KILIMANJARO
|
ECA
|
Wavulana Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Biashara
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ERIC ROBERT MULOGO
|
TUSIIME
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
2
|
EVART EDWARD
|
KIBAHA
|
PWANI
|
ECA
|
3
|
PETERSON P MEENA
|
MBEZI BEACH
|
DAR ES SALAAM
|
ECA
|
4
|
FRANK BUNUMA
|
KIBAHA
|
PWANI
|
ECA
|
5
|
ABDALLAH A JUMA
|
KAZIMA
|
TABORA
|
ECA
|
Watahiniwa Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Lugha na Sayansi ya Jamii
NA.
|
JINA
|
JINSI
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ASIA IDD MTI
|
F
|
BARBRO-JOHANSSON
|
DAR ES SALAAM
|
HGE
|
2
|
GODLOVE GEOFREY NGOWO
|
M
|
MAJENGO
|
KILIMANJARO
|
EGM
|
3
|
JOHNSON ELIMBIZI MACHA
|
M
|
NJOMBE
|
NJOMBE
|
EGM
|
4
|
HAMISI JOSEPH MWITA
|
M
|
ILBORU
|
ARUSHA
|
HGL
|
5
|
SIA H SANDI
|
F
|
MARIAN GIRLS
|
PWANI
|
EGM
|
Wasichana Watano (05)) Bora kitaifa kwa Masomo ya Lugha na Sayansi ya Jamii
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
ASIA IDD MTI
|
BARBRO-JOHANSSON
|
DAR ES SALAAM
|
HGE
|
2
|
SIA H SANDI
|
MARIAN GIRLS
|
PWANI
|
EGM
|
3
|
JACQUELINE B AGRIPPA
|
MASAMA GIRLS
|
KILIMANJARO
|
HGL
|
4
|
DHULFA A KANGUNGU
|
KOROGWE GIRLS
|
TANGA
|
HKL
|
5
|
ANGELIKA D CHENGULA
|
MSALATO
|
DODOMA
|
HGL
|
Wavulana Watano (05) Bora kitaifa kwa Masomo ya Lugha na Sayansi ya Jamii
NA.
|
JINA
|
SHULE
|
MKOA
|
MCHEPUO
|
1
|
GODLOVE GEOFREY NGOWO
|
MAJENGO
|
KILIMANJARO
|
EGM
|
2
|
JOHNSON ELIMBIZI MACHA
|
NJOMBE
|
NJOMBE
|
EGM
|
3
|
HAMISI JOSEPH MWITA
|
ILBORU
|
ARUSHA
|
HGL
|
4
|
ABUBAKAR HASSANI MSANGULE
|
SWILLA
|
MBEYA
|
HGL
|
5
|
ALEX A MKUNDA
|
KIBITI
|
PWANI
|
HKL
|
MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 ya watahiniwa :
89 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani. Matokeo yao yatatolewa mara watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini.
10 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kurudia Mtihani wa Kidato cha Sita 2014 kwa masomo waliyoathirika.
17 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kurudia Mtihani wa Kidato cha sita, 2014.
WATAHINIWA WALIOBAINIKA KUFANYA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI
Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani ya mtahiniwa mmoja (01) washule na watahiniwa watatu (03) wa Kujitegemea waliobainika kufanya udanganyifu katika Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2013.
KUANGALIA MATOKEO YA MITIHANI
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika Februari 2013 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
www.moe.go.tz, na
Dk. Charles E. Msonde
Kny KATIBU MTENDAJI
31/05/2013
picha kwa hisani ya father kidevu blog
picha kwa hisani ya father kidevu blog
No comments:
Post a Comment