Sunday, June 9, 2013

PICHA ZA TUKIO LA KUPANDISHWA CHEO KWA SULEIMAN KOVA KUTOKA NAIBU KAMISHNA KUWA KAMISHNA


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Kamishna wa Polisi (CP) Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye hapo awali alikua Naibu Kamisha wa Polisi (DCP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka cheo cha Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polis, Thobias Andengenye ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi al Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema akimvisha cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Alice Mapunda ambaye hapo awali alikua Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP). Hafla hiyo fupi imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk, Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wawili kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na maofisa kumi na tisa kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP) Suleiman Kova akijipongeza baada ya kuvishwa cheo hicho cha Kamishna wa Polisi (CP) na Mkuu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi al Polisi

No comments:

Post a Comment