WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA
JAMII IMEKABIDHI
MAGARI MANNE KWA MIKOA
MIWILI YA SHINYANGA NA RUKWA
KWA KILA MKOA KUPATA MAGARI MAWILI
YA KUBEBEA WAGONJWA AINA YA TOYOTA
LANDCRUZA , MAGARI HAYO AMBAYO NI
AMBULANCE YATATUMIKA KWA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA VITUOA VYA AFYA..
AKIKABIDHI FUNGUO
ZA MAGARI HAYO KAIMU KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII ,BWANA DONARD MMBADO ,AMESEMA MAGARI HAYO
MANNE , YAMEPATIKANA KUTOKANA NA MICHANGO YA WAFADHILI KAMA CIDA NA PLAN INTERNATIONAL , MAGARI HAYO
MANNE YAMEGHARIMU DOLA LAKI MBILI, SAWA NA PESA TASLIMU ZA KITANZANIA
,MILIONI 320 ILI YATUMIKE KATIKA
MAENEO YA MRADI, SERIKALI ITASIMAMIA GHARAMA ZA UENDESHAJI PAMOJA NA KULIPA
MADEREVA WA KUENDESHA MAGARI HAYO.
MAGARI HAYA YA WAGONJWA YATAWEKWA KATIKA VITUO
VYA AFYA ,ILI KUBORESHA HUDUMA YA AFYA NA DHARURA KWA WAJAWAZITO, WATOTO WACHANGA
KAMA IFUATAVYO, KITUO CHA AFYA WAMPEMBE WILAYA YA NKASI RUKWA ,KITUOA CHA
AFYA CHA
MTOWISA ,WILAYA YA SUMBAWANGA
VIJIJINI ,RUKWA ,KITUO CHA AFYA CHA
MWANGIKA,WILAYA YA SENGEREMA MWANZA NA
KITUO CHA AFYA SANGABUYE ,WILAYA
YA ILEMELA MKOANI MWANZA.
MIKOA HII MIWILI KIJIOGRAFIA
IMEKUWA NI VIGUMU SANA KUPATA HUDUMA
HII YA MAGARI YA WAGONJWA ,AMA
KWA HAKIKA ITASIDIA KUPUNGUZA
VIFO VYA WAJAWAZITO ,WATOTO WACHANGA
NA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO.
MRADI HUU UNATEGEMEWEWA ,KUWANUFAISHA
WANAWAKE LAKI TATU WENYE UMRI WA KUZAA,
WANAUME ELFU THEMANINI NA ZAIDI YA
WATOTO LAKI TATU NA ISHIRINI NA
TANO ELFU , KUJENGA AJIRA KWA ZAID YA WAFANYAKAZI ELFU MOJA WA IDARA YA AFYA SERIKALINI KATIKA VITUO VYA AFYA
199 NA KUSAIDIA ZAID YA
WANAJAMII ELFU TANO WA KUJITOLEA
KATIKA VIJIJI MIA TANO KUMI NA SITA , AIDHA MRADI HUU UTWANUFAISHA MOJA KWA MOJA IDADI YA WATU ZAID YA MILIONI MOJA.
No comments:
Post a Comment