Saturday, July 13, 2013

EWURA YATOA KANUNI KUINUA MATUMIZI YA GESI.


BAADA YA KUONA KIASI CHA MATUMIZI  YA NISHAT I YA GESI  KIMESHUKA ,BODI YA  EWURA (Energy and Water Utilities Regulatory Authority )  IMETOA  KANUNI  MPYA  KUHAKIKISHA MATUMIZI YA GESI YANAONGEKA NA HOFU  YA INATOWEKA KWA WATUMIAJI  WA NISHATI  YA GESI ,HAPA NCHI .

PAMOJA NA KUINUA KIWANGO CHA MATUMIZI PIA BODI IMEADHIMIA KUHAKIKISHA MATUMIZI SALAMA YA NISHATI YA GESI KWA KUTOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA NISHATI YA GESI, PIA WASAMBAZAJI WAMEAGIZWA KUBORESHA VIFAA VYA KUTUNZIA GESI.

AKIONGEA NA SUNRISE RADIO MKURUGENZI  WA EWURA BWANA GODWIN SAMWELI  AMESEMA KANUNI HIZI  ,ZILITOLEWA MWISHONI MWAKA JANA NA KUANZA KUTUMIKA  KUANZIA  TAREHE 28 MWEZI WA DESEMBA 2012, KWA MALENGO MAKUU MAWILI , KUINUA KIWANGO CHA MATUMIZI YA GESI NA  KUHAKIKISHA USALAMA KWA WATUMIAJI.

TATIZO KUBWA LILOKUWA LINAKABILA SUALA LA MATUMIZI YA GESI  NI VIFAA VYA KUBEBEA GESI KAMA MITUNGI NA  VIFUNIKO VYA KUFUNGIA HIYO MITUNGI  LAKINI KWA SASA TATIZO HILO LIMEKWISHA BAADA YA MAKAMPUNI MAKUBWA KUINGIA VIFAA VIPYA  NA VYENYE UBORA  MADHUBUTI NA MATUMIZI SALAMA.


PAMOJA NA KANUNI HIZO KUTOLEWA EWURA IMETOA SHERIA KWA MUUZAJI, AWE NA LESENI INAYOMUWEZESHA KUWEZA KUFANYA BIASHARA HIYO, IKIWA NI PAMOJA NA KUTOA TAARIFA KWA BODI YA EWURA JUU YA UPANUZI WA BIASHARA AU UJENZI WA KITUO KIPYA.

No comments:

Post a Comment