Mkurugenzi wa manisapaa ya kinondoni ndani
ya jiji la Dar es salaam, ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wanoafanya
biashara katika maeneo ambayo hayajahalalishwa kukoma mara moja kwa
biashara hizo kabla ya kutekelezwa kwa
sheria kali.
Tamko hilo la mkurugenzi wa manispaa ya
kinondon enginia Mussa Natty ,ameutoa baada ya kutokea kwa matendo kadhaa ya
ukaid kutoka kwa wafanya biashara ,wanaofanya kazi zao katika maeneo yasiyo
rasmi ,huku wakikaidi agizo la serikali la kuwataka ,kuacha kufanya biashara katika
maeneo yasiyo ruhusiwa.
Pamoja na ukaidi huo wa
wafanyabiashara katika maeneo yasiyo
rasmi,kumetokea sintofaham baada ya wafanyabiashara hao wanaofanya biashara
pembezoni mwa barabara na pengine ndani
ya eneo la mradi wa mabasi yaendayo kasi yaani Dat,kufikia hatua ya kuwapiga
mawe askari mgambo wa jiji pindi wanapokwenda kuwatoa kwa nguvu.
Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara hao
huku akitaja kuwa zoezi kali la kuwakamata wale wote wanaokaidi tamko la
kuondoka litaendeshwa na halmashauri ya
manispaa ya kinondoni na watakaokamatwa mali zao zitaharibiwa na wahusika
kuchukiwa hatua kali.
Akifafanua kuwa zoezi hili la safisha jiji
ambalo ameliitaka ni zoezi endelevu amesema litawahusu wale wafanyabisahara
wanaopanga vitu pembezoni mwa barabara,waendesha bodaboda wanaopaki katika
maeneo yasiyoruhusiwa,wafanyabiashara wakubwa wanaopanga vitu barazani,madereva
taxi na wamiliki wa magari mabovu yaliegeshwa pembezoni mwa barabara na maeneo
yasiyoruhusiwa.
Hata hivyo mkurugenzi amewataka
wafanyabiashara wadogowadogo kuelekeza biashara zao katika magulio na masoko
yalioyopangwa kwa ajili yao na kuacha kufanya biashara maeneo yasiyorasmi na
kusababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu
katika maeneo wanayofanyia biashara kwa
sasa.
Baadhi ya meneo ambayo wafanyabiashara
wametakiwa kuondoka mara moja ni katika eneo la kituo cha mabasi madogo ya
ubongo,kituo cha mabasi madogo mwenge,maeneo yote ya barabara panapoendelea
ujenzi wa barabara ya mabais yaendayo
kasi au mradi wa Dart unaendelea katika barabara ya morogoro,eneo la Manzese na
Tegeta.
Mkurugenzi wa manisaa ya kinondoni enginia
Musa ,Amemalizia kwa kusema anawataka wafanyabiashara kuhamisha biashara zao
mara moja kutoka katika maeneo yasiyo ruhusiwa
na kwenda maeneo elekezi kama
soko la makumbusho na soko la mburahati na wale watakao kaidi agizo hili
watachukuliwa hatua kali za sheria.
No comments:
Post a Comment