Monday, July 8, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA INDIA, SPIKA WA BUNGE LA KOREA YA KUSINI NA AAGANA NA BALOZI WA UHOLANZI


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Uholanzi Mhe.Dkt.Ad Koekkoek anayemaliza muda wake wa uakilishi nchini. Balozi huyo baadaye alifanya mazungumzo na Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Spika wa bunge la Korea ya Kusini Mhe.Hee Chang wakati  spika huyo na ujumbe wake walipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Spika wa Bunge la korea ya Kusini Mhe.Hee Chang baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Spika wa bunge la Korea Mhe.Hee Chang (kulia) akimfurahia  Simba aliyekaushwa na kupamba lango la  ikulu  leo asubuhi. Kushoto ni mwenyeji wake,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur(wapili kushoto) na ujumbe wake  ikulu jijini Dar es Salaam leo.kulia ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe(picha na Freddy Maro) 

No comments:

Post a Comment