Monday, July 8, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 32 WA WADAU WA POSTA KWA NCHI ZA AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine (kulia) na Prof. John Nkoma, Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (wa pili kulia), wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Julai 8, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua rasmi mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha. 
 Kikundi cha Kwaya cha Jijini Arusha kikitoa burudani.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kufungua mkutano huo.

habari kwa hisani ya fatherkidevu blog.

No comments:

Post a Comment