Monday, July 8, 2013

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA UHUSIANO WA KIMATAIFA WA TANZANIA MH. BENARD MEMBE AMEFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI KUJADILI MASUALA YA USHIRIKIANO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA INDIA MH .MRS PRENEET KAUR LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission-JPC) kati ya Tanzania na India unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro kuanzia tarehe 08 hadi 09 2013. Mkutano huo unaowashirikisha Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini na India utajadili pamoja na mambo mengine masuala ya ushirikiano katika sekta za Uchumi, Ufundi, Sayansi na Teknolojia, Elimu, Afya, Utalii, Kilimo na Nishati na Madini.

Wadau kutoka sekta mbalimbali za hapa nchini  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.

Wadau wengine wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau kutoka India.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya India, Mhe. Preneet Kaur akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Kaur (hayupo pichani)

Wadau zaidi.

Meza kuu kabla ya ufunguzi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza machache kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo. Anayeonekana pembeni ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India.

Wajumbe wa Sekretarieti wakati wa mkutano huo.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India.

Mhe. Membe na Mhe. Kaur walioketi, katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga (kulia) akiwa na Mjumbe kutoka India wakati wa Mkutano huo.
Picha na Reginald Philip na Olga Chitanda.
Serikali ya Jamhuri ya muungano na serkali ya India ,wamekutana katika mazungumzo ya Uhusiano ya ushirikiano ,katika biashara,uwekezaji,elimu,afya,utamaduni sayansi ,tecknolojia na habari ili kupanga maeneo ya ushirikiano katika mkutano unaoendelea jijini Dar es salaam.

Akifungua mkutano huo wa mazungumzo utakofanyika kwa siku mbili,Waziri wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ,mh.Benard Membe ,amesema mazungumzo hayo,yanawashirikisha wataalam kutoka jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya India,kwa lengo kubwa la kujadili na kufikia maamuzi,juu ya maeneo ya ushirikiano chini ya viongozi wa mambo ya nje na mahusiano na mwisho wa mkutano huu wa siku mbili ni kutiliana sahihi kwa yale ambayo watakuwa wamekubaliana kushirikiana.

Akifafanua juu ya mazungumzo hayo ,Mh. Membe amesema leo watawasilisha ombi kwa serikali ya India  na kwa makampuni ya mashirika ya ndege ,juu ya kurudisha huduma za usafiri wa ndege kwenda India na kurudi hapa Nchini.


Ombi la kurudishwa kwa huduma za usafiri wa ndege za nchini India zinakuja kwa wakati muafaka kwani Tanzania hivi sasa inaonekana kuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa wanaosafiri kwenda nchini India ila kupata matibabu,ambapo kwa mwaka 2012  peke yake kulikuwa na wagonjwa 2500,  waliokwenda nchini India kupata matibabu.

Pamoja na ombi la kurudisha kwa usafiri  wa ndege hizo za nchini India ,pia mkutano huo  utapata fursa ya kujadili ujenzi wa hospitali kubwa kama ya huko nchini India hapa nchi ili kutoa fursa kwa wagonjwa wenye hali ya chini  kuweza kupata matibabu stahili hapa hapa nchini.

Mh.Membe amesema pia watazungumza juu ya kuomba serikali ya India kuwaunga mkono ,ili kupata fursa ya kuweza kuwania kuingia katika nafasi Mbili za kudumu  katika baraza la usalama wa umoja wa mataifa.

Nae akiongea na waandishi wa habari ,waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa nchini India Mh.*mrs* preneet Kaur amewpmshukuru sana waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. Membe na kuahidi kuwa balozi  wa masuala ya utalii mara baada ya jana kupata nafasi ya kutembelea mbuga ya wanyama ya selou ,ambapo alijionea hali halisi na haiba nzuri ya mbuga hiyo.


Mkutano huo utaendelea mpaka siku ya kesho ambapo mawaziri hawa watapata fursa ya kusain mikataba juu ya yale waliyoafikiana na baadae mh. Waziri atafanya mkutano na waandishi ili kueleza kwa kina juu ya makubaliano hayo hapo kesho.

No comments:

Post a Comment