Shaweji Mketo Naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge katikakati akiwa na viongozi wa Mtwara kulia mwenye shati nyekundu ni SALUM KHAMIS mwenyeikit wa cut Mtwara, na kushoto Said Isa Kulaga katibu wa Cuf wilaya ya Mtwara Mjini hawa wote walitekwa na kuteswa katika kambi ya jeshi huko Naliendele Mtwara na Jeshi la wananchi wa Tanzania wakitakiwa kuonyesha au kumtaja kiongozi anayetuma huko kufanya vurugu.
waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya hali ya mtwara ya kutekwa kwa viongozi wa CUF na kuteswa huko katika kambi ya Naliendele Mtwara.
waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya hali ya mtwara ya kutekwa kwa viongozi wa CUF na kuteswa huko katika kambi ya Naliendele Mtwara.nami pia niliwakilisha chombo changu katika mkutano huo nipo kulia mwisho kwa mbele.
viongozi wa cuf Mtwara wakionyesha makovo ya kipigo walichopata mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijjini Dar es salaam amara baada ya naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge Shaweji Mketo alipomaliza kusimulia hali mkasa mzima wa kutekwa na kupigwa kwao huko Mtwara na wanajeshi wa jeshi lwa wananchi Tanzania

Juzi Jumatano tarehe 26 Juni 2013
Mkurugenzi wetu wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge mhe. Shaweji Mketo alitumwa
na chama chetu kuhudhuria kesi inayowakabili viongozi mbalimbali wa CUF katika
mahakama ya Mtwara Mjini (Kesi inayomkabili MHE.KATANI AHMAD KATANI na
wenzake).
Kwa mujibu wa sheria hata
ikitokea mazingira ambayo hayakwepeki kwa askari wa jeshi au vikosi vingine
kumkamata raia, ni sharti la kwanza kuwa lazima wamkamate raia huyo bila nguvu
na wamkabidhi raia huyo kwa jeshi la polisi mara moja. Sasa iweje Mketo na
wenzie wakamatwe na wanajeshi (kinyume na sheria na bila kufanya kosa lolote)
saa 11 jioni eneo ambalo ni kilometa tatu tu kutoka kituo kikuu cha polisi
Mtwara mjini na badala yake wanapelekwa kwenye kambi ya jeshi kuhojiwa kuteswa
na kushikiliwa? Leo jeshi la ulinzi ndiyo lina kazi ya kuhoji raia?
Tunataka serikali na jeshi
viwajibike haraka iwezeikanavyo. Jeshi la Ulinzi liache mara moja vitendo vya
kinyama vya kuteka na kutesa wananchi wa Mtwara na viongozi wa CUF na tunataka
wanajeshi wamuachie mhe. Mketo na viongozi wetu mara moja na bila masharti
yoyote.
Tunalitaka pia jeshi la polisi
lifanyie kazi ukatili aliotendewa binti ya Selemani
Omari kwa kubakwa na askari jeshi na askari husika afuatiliwe na sheria za
nchi zichukue mkondo wake. Sambamba na hilo ,asasi za kiraia, za kisheria na za
kutetea haki za wanawake zifanye juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wanafika
Msimbati na kukutana na binti huyu aliyebakwa ili asaidiwe kisaikolojia kwani
kitendo alichofanyiwa ni kovu la kudumu kwa maisha yake. Chama Cha Wananchi CUF
kinatoa pole kwa binti aliyebakwa na familia yake, wawe watulivu na wasaidiane
na kila mdai haki kupigania haki yao.
waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya hali ya mtwara ya kutekwa kwa viongozi wa CUF na kuteswa huko katika kambi ya Naliendele Mtwara.
waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya hali ya mtwara ya kutekwa kwa viongozi wa CUF na kuteswa huko katika kambi ya Naliendele Mtwara.nami pia niliwakilisha chombo changu katika mkutano huo nipo kulia mwisho kwa mbele.
viongozi wa cuf Mtwara wakionyesha makovo ya kipigo walichopata mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijjini Dar es salaam amara baada ya naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge Shaweji Mketo alipomaliza kusimulia hali mkasa mzima wa kutekwa na kupigwa kwao huko Mtwara na wanajeshi wa jeshi lwa wananchi Tanzania
viongozi wa cuf Mtwara wakionyesha makovo ya kipigo walichopata mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijjini Dar es salaam amara baada ya naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge Shaweji Mketo alipomaliza kusimulia hali mkasa mzima wa kutekwa na kupigwa kwao huko Mtwara na wanajeshi wa jeshi lwa wananchi Tanzania
viongozi wa cuf Mtwara wakionyesha makovo ya kipigo walichopata mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijjini Dar es salaam amara baada ya naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge Shaweji Mketo alipomaliza kusimulia hali mkasa mzima wa kutekwa na kupigwa kwao huko Mtwara na wanajeshi wa jeshi lwa wananchi Tanzania
viongozi wa cuf Mtwara wakionyesha makovo ya kipigo walichopata mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijjini Dar es salaam amara baada ya naibu mkurugenzi wa mipango ,siasa na bunge Shaweji Mketo alipomaliza kusimulia hali mkasa mzima wa kutekwa na kupigwa kwao huko Mtwara na wanajeshi wa jeshi lwa wananchi Tanzania
Naibu Myweketi wa mipango siasa na bunge Shaweji mketo jana ameongea na wanaandishi wa habari jijini Dar na kuelezea mkasa mazima wa kutekwa kwa na wanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ na kupelekwa katika kambi ya kijeshi ya Naliendele kisha kupigwa ,kuteswa na kudhaililishwa kwa kuvuliwa nguo zote kicha kuchapwa kama mateka na wanajeshi hao.
Akielezea tukio hilo lilotokea manao tarehe 26/06/2013 viongozi mbali mbali walitekwa huko Mtwara walipokuwa wakitekeleza masuala ya kichama soma taarifa hiyo hapo chini inayoelezea mkasa huo ambapo gazeti hili ilichapisha siku zilizopita na leo imekuletea picha na muendelea wa kudhibitisha taarifa hii hapa chini
TAREHE 28/06/2012
KUTEKWA KWA NAIBU MKURUGENZI WA OGANAIZESHENI UCHAGUZI
NA BUNGE WA CHAMA CHA WANANCHI CUF TAIFA MHE. SHAWEJI MKETO NA VIONGOZI WENGINE
WA CUF MKOANI MTWARA.
Mhe. Mketo alipotoka mahakamani
alifanya kikao na wanachama wa CUF Mtwara mjini ambao walimueleza unyanyasaji
na ukatili mkubwa ambao wanajeshi na polisi wanawafanyia wananchi wa Mtwara.
Palitolewa ushahidi wa binti mmoja aliyenajisiwa na binti huyo aliripoti tukio
husika katika kituo cha polisi cha Msimbati kilichoko Mtwara na binti huyo
alipeleka polisi hadi ushahidi wa wa mipira ya kiume iliyotumika kumfanyia
unyama huo lakini polisi hawakuchukua hatua yoyote hadi leo.
Mhe. Mketo na viongozi wengine
waandamizi watano walielekea maeneo ya kijiji cha Msimbati ambako binti huyo
amesitiriwa baada ya unyama huo. Mzazi wa binti aliyebakwa anajulikana kwa jina
la SELEMANI BIN OMARI. Mhe. Mketo na viongozi aliokuwa nao walifika kijiji cha
Msimbati na kukusanya ushahidi walioufuata na kisha wakakutana na wakakutana na
mwenyekiti wa kijiji cha Msimbati ambaye anatoka Chama Cha Wananchi CUF
wakafanya naye kikao kifupi na kisha wakaondoka kurejea Mtwara Mjini.
Kati ya saa 11.30 – 12.00 jioni
walifika eneo la kilometa tatu kabla ya kuingia mjini(Eneo la njia pacha).
Magari mawili ya kijeshi moja likiwa aina ya TATA na lingine likiwa DEFENDER ya
jeshi yaliziba barabara. Ilibidi gari ya mhe. Mketo iliyokuwa ikipeperusha
bendera ya chama chetu isimame(Gari hii ni aina ya NISSAN PATROL yenye namba T
866 BGW – Mali ya Chama Cha Wananchi CUF). Askari jeshi zaidi ya 50 waliivamia
gari yetu na kuanza kuwapiga mhe. Mketo na wenzie bila kuwajulisha chochote na
kisha kuwatupa katika karandinga la jeshi kama vile wanatupa mizigo.
Baada ya kuwateka waliwapeleka
katika kambi ya jeshi ya NALIENDERO iliyoko maeneo ya jirani na Mtwara mjini na
kuwashikilia huko tangu jana jioni hadi leo mchana.
Mimi binafsi nilifikishiwa
taarifa hizo na Mhe. Mtatiro majira ya saa 2 usiku na nilipopewa taarifa hizo
nilipiga simu za mhe. Mketo (Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na
Bunge CUF taifa) na Mhe. Kulaga(Katibu wa Wilaya) na namba zao zilikuwa
zinapokelewa na wanajeshi hao huku wakijibu matusi. Taarifa tulizonazo ni kuwa
Mh. Mketo na wenzie wanateswa na ndiyo maana simu zao zikipigwa wanajeshi hao
watesaji wanajibu matusi.
Mhe. Mtatiro alimpigia RPC wa
Mtwara na RPC akajibu kuwa yeye hana taarifa na viongozi wetu kushikiliwa na
hajui wako wapi. Tumeendelea kuwajulisha viongozi mbalimbali wa jeshi la polisi
na ulinzi juu ya tukio hili. Hivyo, pamoja na mashuhuda kuona wakipelekwa
katika kambi hiyo ya jeshi bado kama chama hatujui hasa wako wapi kwani simu zao zinapokelewa na
watekaji na watesaji wao tu.
CUF – Chama Cha Wananchi
kimesikitishwa na kufadhaishwa na kitendo hiki cha utekaji nyara viongozi na
raia wasio na hatia yoyote. Tumeumizwa zaidi kaa chama baada ya kuona kuwa
jeshi la Ulinzi la Tanzania lenye mamlaka ya kulinda mipaka ya nchi hivi sasa
limeachiwa sasa kazi ya polisi ya kukamata raia. Pamoja na Jeshi kuachiwa kazi
za polisi(JAMBO AMBALO NI KINYUME NA SHERIA), wanajeshi hao wanatumia mamlaka
hayo batili kuteka wananchi, kuwapeleka kwenye kambi za jeshi na kuwateka kwa
siku watakazotaka. Nchi yetu inaelekea wapi? Leo Tanzania mwananchi anakamatwa
na askari Jeshi badala ya polisi! Haya mamlaka askari jeshi wamepewa na nani na
wameyatoa wapi?
Tayari tumewasiliana na
wanasheria wetu tokea jana usiku na timu yetu ya mawakili iko Mtwara Mjini
tangu asubuhi hii kufuatilia suala hili na kuhakikisha kuwa viongozi wetu
wanapata haki. Tunaitaka serikali isiendeleze vitendo vya namna hii kwani
vinawavunja moyo wananchi na vinawakatisha tamaa na hali hii ikiendelea
wananchi watavichukia vyombo vya ulinzi na usalama, jambo ambalo litakuwa na
mustakabali mbaya.
Aidha tunatoa wito kwa vyombo vya
habari vifanye juhudi kubwa kuweka kambi Mtwara ili kujionea ukatili
wanaofanyiwa wananchi na kuuripoti kwa watanzania wote, wananchi wa Mtwara
wasitengwe na asasi zinazoweza kutangaza ukatili wanaofanyiwa.
Imetolewa na :-
Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti wa CUF-Chama cha wanachi, taifa
Mh.Prof.Ibrahim Lipumba
JANA MHESHIMIWA MKETO AMETOA MAELEZO YOTE TANGU KUTEKWA KWAKE HADI KUACHIWA AKIWA YEYE PAMOJA NA WENZAKE AMABAO HAPO JUU NIMEWEKA PICHA ZAO HAKIKA MSOMAJI WA BLOG HII UMEJIONEA MWENYEWE NA KUTAMBUA UFUATILIA NA UKWELI WA HABARI HII DAIMA TUWE PAMOJA KATIKA KULINDA AMANI NA KUTETEA HAKI
WAKATI HUO HUO CHAMA CUF KIMESEMA KITAWAFUNGULIA MASHITAKI WANAJESHI WALIO HUKI KATIKA TUKIO HILI KAMA INAVYOFAFANULIWA HAPA CHINI
CHAMA cha Wananchi (CUF) kinakusudia kulishitaki Jeshi wa Wananchi la Tanzania (JWTZ) kutokana baadhi ya askari wa jeshi wa kambi ya Naliendele mkoani Mtwara kuwakamata kuwapiga na kuwatesa viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.
Tukio hilo lililohusishwa na vurugu za kugombea gesi baina ya wananchi wa Mtwara na Serikali lilitokea Juni 27,mwaka huu ambapo viongozi hao walikwenda kwenye kijiji cha Msimbati umbali wa km 40 hadi 45 kutoka Mtwara mjini kwa lengo la kuthibitisha madai ya mmoja wa wanachama wa CUF anayedai kubakwa na mwanajeshi mmoja.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana, Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Bunge Shaweji Mketo alisema tukio la kubakwa kwa mwanamke huyo ni la kweli,kwani baada ya tukio hilo alichukuliwa na mwenyekiti wa kitongoji na kupelekwa polisi ambapo alipatiwa fomu namba tatu kisha alikwenda hospitali kupatiwa matibabu.
Alifafanua kuwa baada ya kujiridhisha huko waliondoka eneo la Msimbati ambapo robo km(1/4) kutoka eneo la hilo njia panda ya Newala walikuta magari mawili aina TATA na gari dogo mali ya JWTZ yaliyokuwa yamepaki kwa mtindo wa V na kuziba barabara hali iliyosababisha dereva wao Kashinde Kalungwana kusimama kwa lengo la kupisha magari hayo.
Alieleza kuwa baada ya gari lao kusimama walitokeza wanajeshi kama 60 na kuwazunguka ambapo mmoja wao aliyekuwa na cheo cha Kanali alifungua mlango wa gari na kumtoa kisha kuchukua fedha zilizokuwa kwenye mfuko wa shati lake kiasi cha sh.85,000.
"Baadaye msafara wote uliokuwa na watu sita tulipandishwa kwenye gari la jeshi kisha wakanivua viatu vyangu kisha wakanivalisha vya jeshi,walipotufikisha kwenye kambi ya Naliendele walituvua nguo zote kisha tukafungwa kwenye miti iliyopo eneo hilo na kuanza kuchapwa maeneo mbalimbali ya miili yetu isipokuwa kichwani tu,"alisema Mketo.
Alisema kuwa baada ya kujeruhiwa kutokana na kipigo kilichotembea kila baada ya dakika tano waliwekewa maji ya baridi yenye chumvi,ndimu na pilipili kwenye majeraha hayo na baadaye kuendelea na kipigo hadi pale alipopoteza fahamu na kuzinduka saa 11 alfajiri ambapo alijikuta akizungukwa na wanajeshi saba.
"Wanajeshi hao walipokuwa wakitupiga baadhi yao walikuwa wakisema lazima tuwapige kwani heri wachache wafe ila nchi iwe salama,ikiwa wanajeshi wanahamu ya kupigana wapelekwe huko Darfur Sudan au Demokrasia ya Kongo wakapigane na wanajeshi wenzao badala ya wananchi wasio na hatia,"alisema.
Alibainisha kuwa baada ya hapo wanajeshi hao waliwaita askari polisi ambao walifika kwenye kambi hiyo na kuwapeleka kituoni kwa lengo la kutoa maelezo ambapo pia walikataa kuwapa fomu namba tatu kwa ajili ya matibabu kwa madai kuwa haina ulazima wa kupatiwa matibabu.
Mketo alisema baada ya taratibu za polisi kumalizika walifikishwa mahakamani saa 11 jioni ambapo polisi walilazimika kumpigia hakimu simu ili aje kuwasomea mashitaka kutokana na muda wa kazi wa mahakama kumalizika saa tisa na nusu hivyo shughuli hiyo ilifanyika kinyume na sheria za nchi.
Hata hivyo alidai ukiukwaji wa sheria uliendelea kuwepo kwenye mlolongo mzima wa kadhia hiyo kwani watuhumiwa hao walifikishwa gerezani saa 12 jioni ikiwa ni kinyume na matakwa ya sheria.
Aidha alibainisha kuwa watuhumiwa hao walishindwa kupokelewa gereza la Lilungu kutokana na hali mbaya ya kiafya waliyokuwa nayo jambo lililomlazimu Mkuu wa gereza hilo kuwataka askari polisi waliowafikisha gerezani kuhakikisha wanapatiwa matibabu.
"Tunamshukuru Mkuu wa gereza ambaye alikataa kutupokea kutokana na hali zetu,hapo ndiyo polisi wakatupeleka hospitali ya Mkoa Ligula ambapo hatukufanikiwa kupata dawa yoyote zaidi ya dereva wetu kupatiwa kamba ya kutundikia mkono wake kwani ulikuwa umeteguka,"alisema Mketo.
Alibainisha kuwa wananchi wanaumia kwani wanapigwa bila sababu za msingi huku serikali ikichukulia kupigwa kwao kama harakati za kisiasa.

No comments:
Post a Comment