Tuesday, July 9, 2013

WANANCHI TUKATAE KODI YA LAINI YA SIMU YA SHILING 1000 KWA KILA MWEZI -MH ZITTO KABWE

                                                                         Mh.ZITTO KABWE (picha na maktaba yetu)
Ndugu mtanzania  hebu soma na tafakari juu ya kodi ya laini ya simu ya shilingi 1000 kila mwezi kama ilivyo chambuliwa na kuelezwa na mheshimiwa zito kabwe ambaye  ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni.

Kodi ya SimKadi ya tshs 1000 kwa mwezi kwa kila mwenye simu ilikuwa kwenye hotuba ya Bajeti (tshs 1470). Waziri wa Fedha akaliambia Bunge kuwa hiyo imefutwa (alikuwa ametoka kwenye Cabinet kabla ya hapo, hivyo Cabinet haikupitisha kodi hii).

Katika Mjadala wa Bajeti wa wiki nzima kodi hii haikujadiliwa kabisa maana ilikuwa imeondolewa katika mapendekezo ya Mapato. Kodi hii ikarejeshwa Bungeni kupitia Muswada wa Fedha. Muswada wa Fedha hutafsiri hotuba ya Bajeti kisheria.

Kama Kodi hii haikuwa kwenye Hotuba, haikujadiliwa na Bunge, msingi wa muswada wa fedha kuwa na kodi hii haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela Bungeni na kupitishwa bila mjadala. Kodi hii ni batili.

Kodi hii inakwenda kinyume na msingi wa kodi kwani ni REGRESSIVE in nature. Rafiki yangu Mohamed Mohammed Dewji mmoja wa matajiri wakubwa Afrika, atalipa sawa na dada yangu Salima anaetembea jiji zima kila siku kuuza mihogo mibichi. 

Nashawishi wananchi kwa namna wanavyojua waikatae kodi hii mpaka itakapofanyiwa marekebisho makubwa. 
Wananchi wanataka kampuni za simu zilipe corporate tax na sio kuwakamua masikini.

No comments:

Post a Comment