MNAMO TAREHE 04.08.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
NA MBEYA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment