Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard
Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za
madawa ya kulevya aina ya heroine.
Kijana Leonard Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroine.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na vyombo vya habari leo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya. Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremia Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake. Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Badhi ya wanahabari wakimsikiliza Dk. Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
No comments:
Post a Comment