Monday, September 23, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, Nape Nnauye wazuru kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaue akiweka shada la maua wwakati msafara wa KatibuMkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ulipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Mwitongo, wilayani Butiama, Mkoa wa Mara .Kinana na Nape yupo ziarani katika mikoa ya Shnyanga,Simiyu na Mara, kuimarisha uhai wa chamana kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama.

Kinana  akiwa na mtoto wa kwanza wa Bab wa Taifa Hayati Julius Nyerere, Andrew Nyrere (kulia), baada ya kuzuru kaburi la mwasisi wa taifa la Tanzania.Kushoto ni Katibu wa Itikadi na  Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Kinana akiagana na Andrew

Banda ambamo umelazwa mwili wa Baba wa Taifa Hayati Nyerere katika  Kijiji cha Mwitongo
Balozi wa Shina namba namba 14, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama,Safari Zuga  akifungua kikao cha mkutano wa wananchama wa shina hilo ambao Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alihudhuria. Balozi huyo alimsifu Kinana kwa uadilifui wake wa kuamua kuwatembelea mabalozi wa mashina na kutaka vingozi wengine waige mfano huo.
Balozi  mwingene wa shina la CCM, Joseph Mahinya akiuliza swali kwa Kinana katika mkutano huo.
Nape akisalimiana na mama mzazi wa  mwandishi wa habarfi mwandamizi, Jackton Manyerere katika Kijiji cha Mwitongo ,Butiama. Jackton ni Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri.
Nape akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Nimrod Mkono  katika mkutano wa wanachama wa shina namba 14 la Safari katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama.
Kinana akisaidiana na fundi Mgendi Sikila  kupiga plasta katika jengo la Zahanati ya Misegwe ambao Mbunge Mkono amechangia mabati milango na malumalu.
Katibu Mkuu wa UIWT, Amina  Makilagi akisaidia ujenzi wa zahanati hiyo
Nape akihutubia baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo.
Mkono akikabidhi malumalu kwa Kinana tayari kutumika katika ujenzi huo
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi  walihudhuria wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa zahanati hiyo
Wasanii wa ngoma ya jadi wakitumbiza wakati msafara wa Kinana ukiwasili katika Kijiji cha Mazami kuweka jiwe la Msingi ofisi ya Kata ya CCM ya Mazami.
Kinana akisalimiana na mmoja wa wasanii wa kikundi cha ngoma.
Kinana akilakiwa kwa shangwe katika Kiji cha Bwai ambapo alikagua ujenzi na ukarabati wa Shule ya Bwai.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mabula akisalimia wananchi wa Bwai 'Paris'wakati wa mkutano.
Kinana na Mkono wakikagua shule hiyo ambao ujenzi na ukarabati wake kwa kiasi kikubwa umegharamiwa na Mkono ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Wananchi wakishangilia kumlaki Kinana  alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Madaraka, Kyabakari wilayani Butiama.
Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.ambapo aliwaponda wapinzani kwa kitendo cvhao cha kutaka kuharibu mchakato wa Katiba mpya.
Kinana akipewa fimbo na kuvalishwa mgolole baada ya kusimikwa kuwa mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila la wazanaki.
Kinana akimkabidhi katibu wa CCM wa Kata ya Butiama  kwa ajili ya kusaidia kurahisisha  utendaji kazi za chama/Pia baiskeli zilikabidhiwa kwa makatibu kata wilayani huo. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment