Monday, September 23, 2013

Maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani mkoani Dar es Salaam


Baadhi ya waandamanaji  wa  wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam kutoka wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni  wakianadamana kuelekea Viwanja vya  Mwembe Yanga leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
Bendi ya Jeshi la Polisi ikiiongoza maandamano ya wiki ya nenda kwa usalama Mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Koplo Ashura Said akifuatiwa na  ASP Mayala Kulwa. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Baadhi ya waandamanaji  wakiwa wanajiandaa tayari kuanza maadamano  (eneo la TAZARA) ya wiki ya nenda kwa usalama leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akipokea maanadamanoya wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam (wa pili kutoka kushoto), wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa maandalizi ya wiki ya usalama barabarani Elifadhili Mgonja. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjemwa akifuatiwa na Makamu Mweyekiti Jerome Ringo. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Askari wa usalama barabarani wakiwa kwenye kwenye pikipiki kwenye maanadamano ya wiki ya usalama barabarani . Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Baadhi ya wajumbe wa maandalizi ya wiki ya usalama barabarani ya mkoa wa Dar es Salaam wakiwasalimia washiriki wa hafla maadhomisho ya usalama barabarani.
Mwenyekiti wa kamati ya maaandalizi ya maadhimisho hayo Elifadhili Mgonja akizungumza na viongozi mbalimbali wa usalama barabarani (Jeshi la Polisi)  madereva na  wananchi katika hafla ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani leo jijini Dra es Salaam. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjemwa akiwasalimia wananchi walihudhuria hafla ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani leo jijini Dra es Salaam. Aliyeshikilia maiki ni Makamu Mwenyekiti kamati ya maaandalizi ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Jerome Ringo leo jijini Dra es Salaam. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
 Baadhi ya madereva waendeshapikipiki maarufu kama “bodaboda” wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (hayupo pichani) kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ikiongozwa na kauli mbiu  “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ikiongozwa na kauli mbiu  “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Kikundi cha polisi wakitumbuiza kwa mindoko ya “makhirikhiri”wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ikiongozwa na kauli mbiu  “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Kamanda wa usalama barabarani wa mkoa wa Dar es Salaam ACP Amiri Konja (kushoto) akishangilia baada ya  Kikundi cha “makhirikhiri” kutumbuiza wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ikiongozwa na kauli mbiu  “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akizindua wiki ya usalama barabarani ikiongozwa na kauli mbiu  “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki, akizungumza na viongozi mbalimbali wa usalama barabarani (Jeshi la Polisi) madereva na  wananchi katika hafla ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani leo jijini Dra es Salaam. Maadhimisho hayo ya naongozwa na kauli mbiu “Usalama barabarani unaanza na Mimi, Wewe na Sisi sote”.

No comments:

Post a Comment