Monday, September 23, 2013

TASWIRA ZA UWANJA MPYA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE.


Picha sita za muonekano wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) baada ya ujenzi kukamilika


Harakati za maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), zimekuwa zikiendelea polepole hali inayowatia shaka wadau wengi wa sekta hii ya usafiri wa anga. Kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo ni jambo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kwani kukamilika kwa jengo hilo kunategemewa kuleta mabadiliko makubwa sana katika huduma zitolewazo na kuleta ufanisi mkubwa katika huduma za usafiri wa anga na hatimae kukuza uchumi wa nchi.


Hivi karibuni wataalamu na mafundi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga jengo hilo, kampuni ya BAM ya Uholanzi, walionekana wakifanya maandalizi ya mwanzo ya ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio baadhi ya maeneo, upimaji wa ardhi na kubandika michoro yenye kuonesha jinsi taswira ya jengo hilo itakavyokuwa.


Mtandao wa Aviationtz umeshare picha zifuatazo zikionyesha maeneo mbalimbali ya jengo hilo pamoja njia za ndege.


Huu ni muonekano kwa upande wa nje ya jengo na nje ya uwanja.



Hapa ni mahali ambapo abiria watakuwa wakisubiri kabla ya kwenda kupanda ndege (Departure Lounge) 


Muonekano wa ndani ya jengo



Jinsi patakavyoonekana kutokea angani



Muonekano wa jengo,njia za ndege na maegesho ya magari.



Upande wa maegesho ya ndege

Ujenzi wa jengo hilo umepangwa kufanyika kwa awamu mbili. Kukamilika kwa awamu ya kwanza kutawezesha uwanja huo kufikia uwezo wa abiria mil 3.5 kwa mwaka tofauti na jengo la sasa ambalo uwezo wake ni abiria mil 1.5 kwa mwaka. Awamu ya pili itaongeza uwezo huo hadi kufikia abiria mil 6 kwa mwaka. Baada ya kukamilika jengo hilo, jengo lililopo sasa (Terminal II) litatumika kwa shughuli za abiria wanaosafiri ndani ya Tanzania tu.


Chanzo: Aviationtz

No comments:

Post a Comment