Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo. (Picha zote na Magreth Kinabo - Maelezo)
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho akizungumza na waandishi wa habari (pichani) leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
Na Magreth Kinabo- Maelezo
KAMISHNA wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho ametoa onyo kwa watu watakaotumia takwimu ambazo ni sahihi wakati wanapotoa taarifa mbalimbali kuwa wawe makini kwa kuwa sheria ya kuwabana iko mbioni.
Aidha Hajjat Amina amesema kwamba kwa watendaji wa Serikali, na wanasiasa watakaotoa takwimu za uongo katika taarifa mbalimbali wajiandae kuong’ooka katika nyadhifa zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamshina huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
“Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 imeshasomwa mara ya kwanza Bungeni ,unasubiriwa kusomwa kwa mara ya pili katika Bunge lijalo. Hivyo itakapokamilika sisi tutapambana na watu wanaotoa takwimu ambazo si sahihi. Kwa watendaji wa Serikali watakaotumia takwimu ambazo si sahihi wakati wanapotoa taarifa mbalimbali mfano tatizo la njaa linawakabili watu kiwango kipi wajiandae kufukuzwa kazi,” alisema Hajjat Amina.
Alisema suala linatakiwa pia kuzingatiwa watu wataotangaza au kuandika,wakiwemo waandishi wa habari takwimu zilizotajwa na mtu bila ya kufanyiwa uchunguzi kupitia mtandao wa ofisi hiyo watachukuliwa hatua kulingana na sheria hiyo.
Hajjat Amina alifafanua kuwa takwimu hizo zitakuwa zitaboreshwa kwa kila mwaka, hivyo aliwataka watu kuzitumia ipasavyo kulingana na taarifa za kila mwaka.
Akizungunzia kuhusu uzinduzi huo, alisema utafanyika Septemba 25, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dares Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Iddi .
Aidha Hajjat Amina aliongeza kuwa ofisi hiyo itato vitabu 2 , kitabu cha tatu kuhusu takwimu za walemavu kifuata kitazinduliwa mwishoni mwa mwezi wa Okctoba na cha nne kitakachoonesha takwimu za kila mkoa, utakuwa na chake.
No comments:
Post a Comment