PAUL JOSEPH AKIWA STUDIO
Wababe wa nchii POLISI ndivyo walivyo nilaza ndni siku 3 bila kufanya kazi yoyote nikiuguza majeraha waliyoniachia siku ya ijumaa mida ya saa 12 jioni nilipo kwenda kumtembelea rafikia yangu Peter maeneo ya Mbulu mjini baada ya kutoka studio na watangazaji wenzangu.
Nilifika pele nikakuta kuna askari wa TANAPA wanafanya operesheni MJINI ya kukamata mbao watu wengi walijaa eneo hilo kushuhudia lakini chakushangaza ni kwamba askari hao walikuwa wakiwapiga watu walio kamatwa maeneo ya mafundi fenicha na kuwapa adhabu za kijeshi wananchi wa kawaida ambao hata kukimbia kwao ni mtiani mzee mmoja aliambiwa croo tena barabara ya vumbi mzee wa watu akajiburuza kwenye vumbi mbele ya raia wakishuhudia manyanyaso hayo.
Nilishuhudia mtu mmoja akipigwa na kitako cha Bunduki kama vile ni gaidi amekamatwa kumbe wapi ni uonevu tuu ulikuwa unaendelea. Basi tukawa tumekaa nje ya duka la Peter tukiangalia yaliyo kuwa yakifanywa na askari hao mara wakaanza kuwakimbiza wananchi waliokuwa wanaangalia ukatili uliokuwa ukifanyika pale kwa kuwachapa na vipande vya mbao ghafla wakaja mpaka pale tulipo kuwa tumekaa sisi nje ya duka wenzangu wote wakakimbia kwakuwa sikuwa na kosa lolote na sikuwa kikazi eneo hilo hivyo askari mmoja akaniuliza duka lako nikamjibu no nilarafiki yangu, Akaniuliza unafanyanini hapa nikamwambia ni mekuja kumsalimia rafiki yangu au nikosa? Akaniuliza unafanya kazi wapi nikamjibu MWANDISHI WA HABARI akasema ahhhaaa tunawatafuta sana nyie akanishika mkono akanivuta mpaka nje ya baraza mara akaja askari mwingine mwenye bunduki akaniambia piga magoti nikamwambia kwa kosa gani?
mwenzake akasema huyu ni mwandishi akasema hujui tulicho wafanya wenzako ngoja tukuonyeshe. yule wa kwanaza akanipiga na mbao mguuni kabla siakaa sawa mwingine akanipiga mguu wa pili nikakosa nguvu ghafla akanipiga mbao ya bega wakati mwingine anataka kunipiga bega lingine kwa bahati nikazuiya na mkono wa kushoto hivyo ukaumia nao. Kati ya askari hao alikuwepo askari wa JESHI LA POLISI MBULU akawa anawaambia mwacheni kwakuwa nilikuwa nimeumizwa haikuwa na maana yoyote na kama wamenijeruhi kwakuwa kosa langu ni mwandishi basi hakukuwa na aja ya kuniacha kwani siwezi kuacha kuandika na kusema uonevu alioufanya.
wakaniinua wakauliza picha ulizo piga ziko wapi nikawajibu sijapiga picha yoyote ( picha hazukuwa na maana kwangu kwakuwa nipi redion)wakanisachi nikawauliza kwani mnatafuta waandishi au operesheni inahusu nini wakaniuliza hujui operesheni kimbunga nia yanani? kwa kweli upande wangu namfahamu kwaka karibu SIMONI SIRO kwa kuwa nilifanyanae kazi kwa muda flani Tanga wakati akiwa mkuu wa polisi pale lakini sio mtu anae weza kuamuru unyanyasaji kama huu.
Basi wakianiachia moja kwa moja nikaenda kuripoti nilicho fanyiwa kituo cha polisi Mbulu ambapo mkuu wa kituo akaniambia andika maelezo niakapewa PF3 nikaenda hospitali ya wilaya nikahudumiwa matibamu ya kwanza kwani miguu yangu yote hasa magoti na bega la kulia na mkono wa kushoto ambao nilikinga mbio isinipige. Mku wa kituo akaniambia niende kesho yake kituoni nikaenda akaniambia nitakupigia simu nini kinaendelea.
NDUNGU ZANGU KWA UPANDE WANGU NASHUKURU MUNGU NAENDELEA VIZURI NA MATIBABU ninacho uliza Je TANAPA walicho kifanya nisawa?
Je operesheni kimbunga ndio lengo lake?
Je uperesheni kimbunga inalenga waandishi wa habari?
Je tanapa wanaruhusiwa kuwapiga wananchi ovyo na kutoa adhabu za kijeshi?
Je walio pigwa na kuumizwa bila ya kutoa taarifa watapataje haki yao, na kuendekeza manyanyaso kwa wananchi?
LAKINI PIMSHUKURU SANA PROGRAME MANAGER WA REDIO HABARI NJEMA KWA KUSHIRIKIANA NAMI NA WAFANYAKAZI WENZAGU KATIKA KIPINDI HIKI NINACHO KIPITIA
KUSHIRIKIANA NAMI NA WAFANYAKAZI WENZAGU KATIKA KIPINDI HIKI NINACHO KIPITIA
Pia pole kwa Diwani wa sanu Mh Ambrosi ambaye naye alikumbwa na masaibu hayo je wananchi wa kawaida watapata haki zao kweli kama imefikia hapa
UONGOZI BLOG HII UNATOA POLE KWA MWANDISHI PAUL JOSEPH KWA YALIYOMKUTA
No comments:
Post a Comment