Wednesday, November 27, 2013

Kongamano la Wasanii kufanyika kesho ukumbi wa Vijana Kinondoni


Mkurugenzi toka Kampuni ya Chief Promotion Amon Mkoga (kulia), akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam, juu ya kongamano la wasanii litakalofanyika kesho ukumbi wa Vijana Kinondoni, jijini. Katikati ni Mkuu wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari toka mfuko wa Pensheni wa PSPF na kushoto ni Msanii wa bongo fleva Jumanne Omary toka kundi la Mabaga Fresh.
Wasanii wa kundi la Mabaga Fresh, Christom Mwingira (Dj Snox) kushoto na Jumanne Omary (JB Mkuu wa Majaji), wakiimba kwa hisia mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam, wakati wakihamasisha juu ya kongamano la wasanii litakalofanyika kesho, Viwanja vya vijana, Kinondoni.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Chief Promotion, Amon Mkoga (hayupo pichani), wakati akielezea juu ya kongamano la wasanii litakalofanyika kesho, Viwanja vya Vijana, Kinondoni jijini. (Picha zote na Eliphace Marwa (Maelezo) 

No comments:

Post a Comment