Saturday, November 23, 2013

Mahafali ya Nne ya UDOM, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Simba Chawene ahitimu Shahada ya pili ya Uzamili katika Uongozi


Naibu waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene  (aliyevaa joho), akiwa katika picha ya pamoja na familia yake kwenye Viwanja vya Chimwaga (UDOM), baada ya kuhitimu Shahada ya pili ya Uzamili katika uongozi. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
Mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika Uongozi, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akipiga makofi kufurahia jambo pamoja na wahitimu wenzake, wakati wa mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), yaliyohudhuriwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, mjini Dodoma leo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Benjamin Mkapa ambaye ni mgeni rasmi katika Mahafali ya Nne ya chuo hicho, akiwa katika hafla hiyo, iliyofanyika Chimwaga mjini humo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Dk. Juma Mwapachu na kulia ni Makamu Mkuu wa chuo, Idris Kikula.
Mlau wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akiongoza maandamano ya wahitimu katika mahafali ya Nne ya chuo hicho, huku akiwa amebeba mfano wa ufunguo kama alama ya Elimu kuwa ufunguo wa maisha.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM, akimtunuku kwa kumvilisha kofia mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Uzamivu (PHD) katika Sayansi ya Jamii, David Mwendamaka kama ishara ya heshima kufikia ngazi hiyo.
Baadhi ya wahitimu wakipiga picha na familia zao, wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wakiwa katika furaha baada ya kuhitimu na kutunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa leo, mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment