Friday, November 15, 2013

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk. Sira azungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Kisukari duniani

Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza (NCD), Omar Mwalim Omar, akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya  wa Zanzibar, Dk. Sira  Ubwa Mamboya, kuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya Siku ya ugonjwa wa Kisukari duniani katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazi Mmoja, mjini Zanzibar leo. 
Naibu waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu siku ya kisukari Duniani katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar kulia ni Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza (NCD) Omar Mwalim Omar. 
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Talib Ussi Hamad akimuuliza swali Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar katika mkutano wake na waandishi wa habari  uliofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja kuhusu siku ya kisukari  iliyoadhimishwa leo Duniani kote.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakitaka ufafanuzi zaidi kutoka kwa Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza (NCD) Omar Mwalim Omar kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani ambapo maadhimisho yake hufanyika kila ifikapo tarehe 14 Nomvemba  ya kila mwaka. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment