Friday, November 8, 2013

TRA yaadhimisha Siku ya Mlipakodi mjini Dodoma


Mkuu wa mkopa wa Dodoma Drk Rehema Nchimbi akimkabidhi cheti mfanyabiashara anayemiliki vituo kadha vya mafuta Karlim  Azizi Banji, katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mlipa kodi nchini. Cheti hicho, kilitolewa na Mamlaka ya Mapato mkoani kama ni kielelezo cha kulipa kodi anayechangia pato la Taifa.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Dodoma, Thadeo Kaliza akifafanua jambo kwa wakazi wa mji huo, waliohudhuria  kushuhudia kilele cha siku ya mlipa kodi yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwa na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa, Thadeo Kaliza (kushoto) na Meya wa manispaa hiyo, Emanuel Mwiliko walipokuwa kwenye maadhimisho ya kilele cha Siku ya mlipa kodi yaliyofanyika Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere, mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwahutubia wananchi wa mkoa huo, waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya kilele cha Mlipakodi yaliyofanyika jana mjini humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akikabidhi cheti cha mlipaji kodi bora kwa Wafanyabiashara wa Kati kwa muwakilishi wa duka la vitabu la Kampuni ya Victory Bookshop,
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walihudhuria maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mlipa kodi, yaliyofanyika jana mjini Dodoma.Sameera Ismail Dawood kwenye katika maadhimisho hayo. (Picha zote na John Banda)

No comments:

Post a Comment