Tuesday, November 26, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda afungua Mkutano wa kimataifa wa watendaji wa Serikali za Mitaa kutoka Tanzania na China jijini Dar leo


 Washiriki wa mkutano wa ushirikiano kati ya watendaji wa ngaza za Serikali za Mitaa wa Tanzania na China pamoja na wafanyabiashara wa sekta binafsi, wakijisajili kabla ya kuingia katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulidhaminiwa na Benki ya CRDB.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa kimataifa wa watendaji wa Serikali za Mitaa kutoka Tanzania na China  uliofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Huduma Shirikishi,Esther Kitoka (katikati), Meneja wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Biashara za Serikali, Nuru Kateti na mmoja wa wakurugenzi wa Benki hiyo, James Mabula wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa mkutano wa ushirikiano wa watendaji wa Serikali za Mitaa wa Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB ilidhamini mkutano huo. 
 Baadhi ya watendaji wa serikali za Mitaa kutoka Tanzania.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu (wa pili kushoto) akifuatilia mkutano huo pamoja na wakuu wenzake wa wilaya.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Huduma Shirikishi, Esther Kitoka (wa pili kulia), akiwa na maofisa wa benki hiyo wakati wa mkutano wa ushirikiano wa watendaji wa Serikali za Mitaa wa Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB ilidhamini mkutano huo.  
 Washiriki wa mkutano huo kutoka China.
Mshiriki wa mkutano wa ushirikiano wa watendaji wa ngazi za Serikali za Mitaa kutoka Tanzania na China akisoma vipeperushi vyenye maelezo ya huduma za Benki ya CRDB wakati alipotembelea benki hiyo kujua huduma wanazotoa. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Ninael Munuo.

No comments:

Post a Comment