Mhe.
Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Mhe.Balozi Amina Salum Ali,Mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini
Marekani (kushoto)na Mhe. Linda Thomas Green- Field,Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje ya Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika (katikati)
Mhe. Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Somduth Soborun, Balozi wa Mauritius nchini Marekani.
Mhe.
Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania(Kushoto)katika picha pamoja na Mhe.Linda Thomas-
Greenfield,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia
masuala ya Afrika(wa pili kushoto) na Mhe. Michael Moussa Adamo, Balozi
wa Jamhuri ya Gabon nchini Marekani(wa pili kulia) na Bw. Suleiman
Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia).
RAIS
Barack Obama amewaalika Marais 46 wa Bara la Afrika katika mkutano wa
kwanza wa aina yake "US-Africa Summit" utakaowakutanisha na viongozi wa
juu wa Serikali ya Marekani na kuweka mkakati endelevu baina ya
Marekani na Bara la Afrika. Mkutano huo wa kihistoria utafanyika katika
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani maarufu State Department Agosti
5-6,2014, Washington DC. Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ni mmoja wa katika ya viongozi kutoka barani Afrika
walioalikwa katika mkutano huo.
Mkutano
wa awali ulioitishwa mwishoni mwa wiki iliyopita uliongozwa na Mhe.
Linda Thomas Green- Field, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
anayeshughulikia masuala ya Afrika aliyeambatana na Bw. Grant Harris,
Mshauri wa Rais Barack Obama katika masuala ya Afrika. Madhumuni ya
mkutano huo ulikuwa ni kuwapa fursa Mabalozi wanaoziwakilisha wa Afrika
wanaoziwakilisha nchi zao hapa Marekani kuchangia masuala muhimu ambayo
wanaona yatakidhi kujadiliwa katika mkutano.
Mabalozi
kadhaa walichangia na kutoa maoni yao akiwemo Mhe. Liberata
Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na
Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Mwakilishi wa Umoja wa Afrika hapa
Marekani.
No comments:
Post a Comment