Mwenyekiti (Taifa)- TYVA. Elly Ahimidiwe Imbyandumi kushoto akiwa na Bwana Frank wa idara ya habari maelezo walipokutana na waandishi wa habari.
|
Tanzania Youth Vision Association (TYVA) ni asasi ya vijana isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kupata usajili wake mwaka 2002 kupitia wizara ya mambo ya ndani, Hivyo Asasi hii haifungamani na chama chochote cha siasa, dini,ukanda ukabila, na malengo yakuanzishwa kwake ilikuwa na malengo makuu mawili Kwanza ni kujenga jamii huru, ya haki na ya kidemokrasia ambamo vijana wana ushiriki wa hali ya juu na makini.
Pili bila kusahau kwa miaka hiyo kulikuwa na ushawishi na ushiriki mdogo wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi hivyo basi lengo pia lilikuwa ni kujaza nafasi iliyokuwa wazi ya kukosekana kwa asasi makini yenye uwezo wa kutetea vijana katika changamoto zao kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni, Pia kushawishi watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi mbalimbali ili kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua na kujiwezesha wao wenyewe bila kuwa tegemezi au kuonekana kama ni mzigo kwa taifa.
Ndugu Wanahabari,Kama sehemu ya kupigania ushiriki na ushirikishwaji wa vijana kwenye kufanya maamuzi ya mustakabali wao na wataifa, mtakumbuka mwaka 2010 kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu TYVA iliandaa AJENDA YA VIJANA ambapo dai la katiba mpya inayojali maslahi ya vijana lilikuwa mojawapo ya madai ya vijana.
Fursa ya kuandika katiba mpya ilipopatikana, TYVA bado iliendelea kusukuma ajenda za vijana kwa kutoa maoni kwa tume kwa mlango wa Asasi za Kirai baada ya kukusanya maoni hayo kutoka kwa vijana mikoani.
Noamba pia kuwajulisha ya kuwa tangu Februari 2011 mpaka Disemba 2012 TYVA imeshiriki michakato yote ya kuandaa katiba mpya ikiwa ni pamoja kukusanya maoni ya vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kuandika katiba Mpya. Tuliwasilisha maoni ya vijana mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 9 Januari 2013 katika ukumbi wa Karimjee.
Tuliunda baraza la Katiba la TYVA tarehe 17 Agosti 2013 na kuwasilisha maoni ya kuboresha rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya tarehe 30 Agosti 2013.
,Kwa hatua ya sasa TYVA inatoa pongezi kwa Tume ya Mabadiliko ya kwa kuweza kutoa rasimu ya pili yenye marekebisho kadhaa ya maoni ya wananchi ukilinganisha na rasimu ya kwanza.
Ni jambo lililo wazi kuwa rasimu ya pili imeweza kuongeza vipengele kadhaa muhimu, mfano ni ibara zinazowapa wananchi mamlaka ya moja kwa moja ya kuwawajibisha viongozi wao, kuweka miiko ya uongozi, Tunu za taifa na utoaji wa huduma za kijamii kwa kila mtanzania kama haki za msingi, Mfumo wa serekali tatu nakadhalika.
Lakini kwa upande mwingine, bado kuna ibara hazijaelezewa kwa mapana i, mfano ni ibara ya 44 inayotulenga moja kwa moja sisi Vijana, Ibara hii imeeelezewa kwa ujumla sana bila kunyambua haki za msingi na wajibu wa vijana kama inavyotakiwa ikilinganishwa na ibara zingine katika rasimu hii ya katiba zinazogusa makundi mengine kama ya watoto(43), wanawake (47) na ya wazee (48).
Ni kwasasababu hii basi TYVA tunashaui makundi yote ya uwakilishi kutoka asasi za kiraiya, wabunge na hasa wabunge vijana kulisemea swala hili na hasa Ibara ya 44 iweze kumwelezea kijana kwa mapana yake katika hali ya kutatua mazingira magumu vijana wanayopitia ya ukosefu wa ajira, huduma rafiki za afya kwa vijana, elimu, ukosefu wa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara,pia uongozi na diplomasia.
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC
Kwa kuwa sheria ya mabadiliko ya katiba inabainisha kuwa kura ya maoni ya katiba mpya itapigwa kwa kutumia dafatari la kudumu la mpiga kura, TYVA inatoa wito kwa tume ya Uchaguz NEC kutoa ratiba ya maboresho ya daftrai hilo mapema iwezekananyo ili kuepusha malalamiko hasa itakapotokea kuwa zoezi hilo litafanyika karibu sana na muda wa kura ya maoni ya katiba.
Ni muhimu kutoa muda wa kutosha kwa zoezi hili kwani NEC haijaboresha daftari hili tangu uchaguzi mkuu wa 2010 na hivyo kupelekea mamilioni ya watanzania hususani vijana ambao walifikisha umri wa miaka 18 tangu 2011.
Ni muhimu NEC ikatambuau si chini ya wiki sita kufanya zoezi hili tofauti na wiki tatu kama ilivyokuwa huko nyuma kwani pia mabaoresho haya ndio yatabeba picha ya wapiga kura wa uchaguzi mkuu 2015.
Ni matumaini ya TYVA kuona bunge la katiba kupitiia kwa wajumbe waliopata bahati ya kutuwakilisha vijana tulio asilimia 65 kati ya idadi ya watanzania wote, hivyo basi tunashauri wajumbe watumie busara zao kujadili kwa kina ibara hii yenye Majumuisho na kijana azungumziwe kwa mapana yake katika swala la Haki na Wajibu tofauti na ilivyo sasa. Pia tunawakumbushi wajumbe wakumbuke bado Vijana wa Tanzania tunakumbana na changamoto za kutokuwapo na ajira zinazokidhi soko la wahitimu wa kila mwaka katika vyuo mbalimbali,
BARAZA HURU LA VIJANA Hiki kitakuwa ni chombo imara sana katika kutunga, kurekebisha na hata kulishauri bunge katika sera rafiki kwa vijana na Taifa zima,
Mwisho kabisa sisi vijana kupitia TYVA tunafahamu changamoto nyingi taifa linazopitia kama vile uongozi mbovu, ukosefu wa ajira, afya, elimu,maji safi na salama, Rushwa iliyokidhiri,Tatizo la umeme, n.k) kwa upande mwingine changamoto hizi huathiri sana maendeleo ya vijana na wananchi kwa ujumla kutokana na matatizo ya kimfumo wa kiutawala tulionao, hivyo upatikanaji wa katiba mpya itakuwa ni mwanzo wa kubadili mfumo huu na hatimaye kutatua changamoto hizi za sasa na zijazo.
Mwisho kabisa, tunatoa shime kwa wananchi, bila kujali tofauti zao, kuendelea kushiriki katika mchakato wa katiba hasa itakapofika wakati wa kura ya maoni ili tupate katiba inayokidhi matakwa ya wananchi wote kwa ujumla wao.
Imetolewa na:
Elly Ahimidiwe Imbyandumi
Mwenyekiti (Taifa)- TYVA.
February 4, 2014.
No comments:
Post a Comment