Afisa utetezi wa haki za kiuchumi wa OXFAM Mkamiti Mgawe akielezea kwa kina namna ambavyo wanafanya mchujo wa kumpata mshiriki wa awali wa mama shujaa wa chakula/ Maisha Plus ambapo washiriki wanatarajia kuingia katika kijiji cha Maisha Plus mwezi wa tatu mwaka huu 2014.
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
Majaji wakuu walioteuliwa kwa ajili ya kufanya mchujo wa kuchagua Mama Shujaa wa Chakula 30 na vijana 45 ambao baadae watafanyiwa usahili na kubakiza wanawake 20 pamoja na vijana 30 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) aliyevaa kofia akipitia kwa umakini Fomu za mchujo za Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus.
Wanafunzi 17 ambao wana fani mbalimbali na waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Tumaini ambao wanawasaidia majaji kupitia fomu za mchujo ili kuwapata wale watakaofanikiwa kuingia katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
Baadhi ya wanachuo wakiwa wanaendelea kupitia Fomu kwa umakini kuhakikisha wanawatendea haki washiriki wote walioleta Fomu zao.
Mmoja wa wanachuo akifanya maheesabu kwa makini ili kutoa alama kwa washiriki walioleta fomu kwa ajili ya mchujo ya kuwapata watakaoingia katika usahili wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula
Baadhi ya Fomu zikiwa zimemalizika kupitiwa na wanafunzi wa Chuo kikuu ili kupelekwa kwa Majaji wakuu.
************
Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki.
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi Alhamisi tarehe 6 Februari 2014. “Majaji walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu.
Baada ya uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45 ambao watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia kuchambuwa fomu na vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Jinsia. “
Jopo la majaji linajumuisha waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii.
Majaji ni kama wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 ; Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha Plus 2012.
Washiriki wa Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha Fedha za kitanzania Milioni 25.

No comments:
Post a Comment