Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mh. Christopha Chiza akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,lililomalizika leo kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.Mh. Chiza amelifunga Kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ambaye hakuweza kuhudhulia kutokana na kubanwa na shughuli nyingi za Kitaifa.Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa siku tatu mfululizo,liliweza kujadili mambo mengi kuhusiana na fursa ya kuwekeza katika Kanda hiyo ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa,Mh. George Kahama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuja kufunga Kongamano hilo lililokuwa likifanyika kwa siku tatu katika Hoteli ya Malaika,Jijini Mwanza.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Chifu Paschal Mabiti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini,Julieth Kairuki akitoa taarifa ya Kituo chake na jinsi wanavyoshirikiana kikamilifu na Wawekezaji mbali mbali wakiwemo wa ndani ya nchi na wale wanaotoka nje ya nchi.ambapo amesema kuwa Kongamano hilo limekuwa ni kama ishara ya uzinduzi wa mkakati endelevu wa kuibua na kunadi fursa mbalimbali zilizopo katika kanda ya ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Ally Rufunga akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wakuu wenzake wa Mikoa ya Kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Mara,Kagera na Geita.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano Uwekezaji Kanda ya Ziwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo akiwahoji wajumbe wa Kongamano hilo kuhusiana na kuwepo kwa Mwenyekiti wa Kongamano hilo,ambaye ni Mh. George Kahama (kulia),ambapo Wajumbe wamempokea vyema Mh. Kahama na kusema kuwa anafaa kabisa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa Kongamano hilo.
Prof. Lazaro Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (Idara ya Sayansi ya Wanyama) akisisitiza jambo wakati akitoa Mada yake kwenye Kongamano la Uwekezaji Kanga ya Ziwa.
Dkt. Kato Peter kutoka Chuo cha IFM akichangia Mada.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh. Abdul Lutavi akichangia mada kwenye Kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa TCCIA,Joseph Kahungwa akichangia mada kwenye Kongamano hilo.
Muwekezaji kutoka Kagera akichangia mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Julieth Kairuki akiteta jambo na Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Mh. Thamduycse Chilliza wakati wa Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment