Thursday, February 20, 2014

MAMIA YA WANAWAKE WAJITOKEZA KUHUDHURIA SEMINA YA MWANAMKE NA AKIBA


Katika kuitikia wito uliotolewa jana na Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali wakati akifungua Tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba, mamia wa kinamama na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, leo walijitokeza kuhudhuria Semina ya Mwanamke na Akiba inayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Dar Live.

Akizungumza katika Semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima alisema kuwa Semina ya Mwanawake na Akiba, ni muendelezo wa siku tatu za Tamasha la Mwanamke na Akiba linalotarajiwa kuzunguka nchi nzima lenye lengo la kutoa elimu kwa akina mama hususani walio katika sekta isiyo rasmi kwani linatoa fursa ya kuwatoa wanawake katika utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato chao.

Aliongeza kuwa muitiko wa wanawake na vijana hao katika semina hiyo, inaonyesha namna wanawake na vijana wa Kitanzania walivyo na nia na dhamira ya kujiongezea ujuzi na kujielimisha kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali. “Washiriki wanatumia fursa hii kwa kujipata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha,” alisema.

Tamasha la Mwanamke na Akiba linakusudia kuwaelimisha wanawake na vijana juu umuhimu wa kuweka akiba, mbinu tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kujiwekea akiba.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akizungumza na wanasemina (hawapo pichani) juu ya lengo la semina hiyo. Bi Naima aliwasihi wanasemina hao kuzingatia wanayofundishwa ili kutimiza malengo yao ya uwekaji akiba. Picha na Salum Sasamalo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Bi Naima Malima akizungumza na Afisa Uhusiano na Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi Agnes Lubuva wakati wa Semina ya Wanawake na Akiba, ikiwa ni muendelezo wa siku tatu za Tamasha la Mwanamke na Akiba.
Tamasha halikuwaacha nyuma wanawake na vijana wenye uhitaji maalum. Pichani ni mtaalam wa lugha za alama alikuwepo kurahisisha mawasiliano na wanasemina wenye ulemavu wa kusikia. Pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi.
Baadhi ya wanawake na vijana walioshiriki Semina ya Wanawake na Akiba.
Baadhi ya wanawake na vijana walioshiriki Semina ya Wanawake na Akiba.

No comments:

Post a Comment