Tuesday, May 6, 2014

Hisia za Pistorius baada ya mauaji

Oscar Pistorius akiwa mahakamani
Mwanariadha anayekabiliwa na kesi ya mauaji nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius alikuwa na majuto baada ya kumuua mpenzi wake.

Hii ni kwa mujibu wa ushahidi wa jirani yake huku kesi dhidi ya mwariadha huyo ikianza kusikilizwa tena baada ya kuahirishwa kwa wiki mbili.

Pistorius amekana madai kuwa alimuua mpenzi wake kwa maksudi.Johan Stander jirani yake Oscar, alikuwa mtu wa kwanza kuja nyumbani kwa Oscar baada ya Oscar kumpiga risasi mpenzi wake marehemu Reeva Steenkamp mwaka jana.

Familia ya Oscar iko mahakamani kumuunga mkono

Anasema kuwa alifyatua risasi kupitia mlango wa chooni wakati akiwa katika hali ya kuogopa akidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Bwana Stander alitaka kuonyesha kuwa Bwana Pistorius' alikuwa na majuto na uchungu mwingi kwa kumuua mpenzi wake na kwa hivyo huenda alimuua kwa bahati mbaya.
"Niliona ukweli asubuhi ile na ninahisi hivyo ndivyo ilivyokuwa,’’ Sanders aliambia mahakama."Alitaka sana kumuokoa na alichofanya tu ni kumuomba Mungu,’’ aliongeza kusema shahidi huyo.
Stander, anayeishi umbali wa mita 350 kutoka nyumbani kwa Oscar, aliitwa nyumbani kwa Oscar punde baada ya mauaji hayo.
Alisema kuwa mwanariadha huyo alimwambia kwamba: ''Nimemuua Reeva nikidhani alikuwa jambazi kavamia nyumba yangu, tafadhali njoo haraka.’’
Bwana Stander alisema kuwa alipowasili nyumbani kwake Oscar alimuona mwanaridha huyo akishuka ngazi akiwa amembeba Reeva.
"Alikuwa analia, akipiga mayowe, akiomba Mungu,’’ alisema Stander naye akiwa analia.
‘‘Sidhani ni kitu ningependa kuona tena maishani mwangu,’’ alisema jirani huyo
Stander aliambia mahakama kuwa eneo hilo lilikuwa limewahi kuvamiwa , ingawa kwa ujumla wake ni mahali salama.

No comments:

Post a Comment