UTANGULIZI
Kanda Maalum ya
Polisi Dar es salaam ina utaratibu wa kufanya mazungumzo na wananchi kwa
kupitia vyombo vya habari vya aina mbalimbali kwa lengo la kuwapasha habari
wananchi kuhusu hali ya usalama jijini na hatua zinazochukuliwa na Polisi Kanda
Maalum ya Polisi Dar es salaam katika kukabiliana na changamoto za uhalifu
jijini na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi husika.
Katika kipindi cha
wiki mbili tangu tulipokutana mara ya mwisho yametokea matukio ya uhalifu ya hapa na pale ambayo
wananchi ambao ni walaji wa huduma za ulinzi na usalama wanatakiwa kupewa
taarifa ili kwa pamoja tushirikiane kupunguza uhalifu jijini au kuutokomeza
kabisa.
TAARIFA YA MAFANIKIO KATIKA UTENDAJI
Matukio
yaliyojitokeza katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ni haya yafuatayo
OPERATION MALUM YA KUZUIA KUPAMBANA NA MATISHIO YA
UHALIFU KUFANYIKA D’SALAAM.
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum linaanzisha operesheni maalum ya kupambana na vitendo mbali mbali
vya uhalifu ambayo vimejitokeza na kuashiria uvunjifu wa amani na kuleta tishio
kwa wakazi wa D’salam.
Matukio yaliyojitokeza
kwa matishio ni kama yafuatayo:-
1.
Ujambazi wa kutumia silaha
2.
Dawa za kulevyaa za viwandani na mashambani
3.
Majambazi wanaoteka na kufanya uhalifu dhidi
ya watu wanaosafirisha fedha taslim kiholela
4.
Majambazi wanaovizia katika mabenki na
maduka ya kubadilishana fedha (Bureau De Change)
5.
Vikundi vinavyojihusisha na itikadi kali kwa
kutumia mwavuli wa Dini, siasa au wahalifu wanaofanya vitendo vinavyoashiria na
kujielekeza katika kufanya ugaidi.
6.
tutapambana na kero ambazo ni vyanzo vya
uhalifu ambavyo ni maeneo yanayojihusha na kusambaza na kuuza dawa za kulevya,
upishi wa pombe haramu ya gongo, baa na grocery yanayokesha na katika pamoja na
wateja wao wakilewa kucha na wale wanaopiga mziki usiku katika mtaa bila kujali
maisha au mapumziko kwa raia wengine wanaoishi jirani.
Operesheni
hiyo imezingatia kumbukumbu za uhalifu ambazo zimeanza kujitokeza wakati wa
mchana na usiku ambapo kama mwenendo huo hautadhibitiwa hali ya utulivu katika
jiji la D’Salaam utavurugika na wananchi wataanza kuishi katika hali ya
hofu. Aidha yapo mawasiliano ya karibu
kati ya Polisi Kanda Maalum na Makamanda katika mikoa ya mipakani ili
kuhakikisha kwamba silaha zote zinazoingia D’Salaam hazivushwi kiholela kwa
njia za panya katika mikoa hiyo na hatimaye kutumika kwa uhalifu katika jiji la
D’Salaam.
Operesheni
hii kali ya aina yake inataendeshwa kwa awamu tatu hadi mwishoni mwa mwaka
huu. Tunatoa wito kwa wananchi waendelee
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili mafanikio makubwa zaidi yapatikane
dhidi ya uhalifu.
MTANDAO
WA WAHALIFU WANAOTUMIA TEKNOLOJIA YA
MAWASILIANO (IT) WAKAMATWA JIJINI DA ES SALAAM
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam limewakamata watu wawili
wanaojihusisha na mtanda wa uhalifu kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano (IT)
ambapo taarifa za kiintelijensia zilionyesha kwamba lengo lao ni kuwasaidia
wahalifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na wale wa kutumia silaha. Pia
imebainika kwamba watuhumiwa hawa huwasaidia watu walioiba simu kwa kubadilisha
kumbukumbu zao ili wasiweze kukamatwa na Polisi.
Watuhumiwa
hawa walikamatwa tarehe 11/09/2014 huko Kariakoo katika mtaa wa Agrey
wakijifanya ni mafundi wa kawaida wa simu ambapo wamesomea teknolojia ya
mawasiliano (Information Technology) katika vyuo vilivyopo jijini Dar es Salaam
kwa sasa ni mafundi wa simu za mikononi ambao hujihusisha na vitendo vya
KUFLASH SIMU, KUFUNGUA PASS WORD, na kupoteza IMEI NAMBA za simu wanazoletewa
na wahalifu kwa lengo la kubadilisha utambulisho (IDENDIFICATION) na uhalisia
wa simu husika.
Majina ya
watuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1.
EDSON
S/O KENNEDY NDEIKYA, miaka 27, fundi simu mkazi wa Mabibo Kanuni.
2.
IBRAHIM
S/O MUHDINI KASUKU, miaka 23, fundi simu, mkazi wa Keko Magurumbasi.
No comments:
Post a Comment